Mtengenezaji wa maudhui ya mtandaoni kutoka Tanzania Mwijaku amewasuta baadhi ya wasanii wa taifa hilo kwa kukosa kujitokeza kwa hafla ya Marioo ya kuzindua albamu yake mpya kwa jina The Godson.
Mwijaku kupitia ukurasa wake wa Instagram kweney kitengo cha matukio yaani Insta Stories amewataja Mwambino, Juma Jux na S2Kizz kwa kukosa kuhudhuria uzinduzi wa albamu ya Marioo iliyofanyika usiku wa kuamkia Jumamosi tarehe 30, Novemba.
Kwa mujibu wa Mwijaku, ametaka kufahamu kutoka kwa watatu hao ikiwa ni chuki au uwoga ndio utaaminiwa.
“Kwa nini hamja msapoti MARIOO wala kutokea kwenye uzinduzi wake? Licha ya yeye kujitokeza kwenye events zenu! Je tuamini kwenye chuki au uwoga?” Aliuliza Mwijaku kwenye Insta stories zake.
Mwijaku ameshangazwa na kukosa kwa Mwambino kujitokeza kwenye hafla hiyo akishindwa kujua ikiwa uaminifu utawekwa kwenye chuki au uwoja wa kufunikwa.
“Je tuamini kwenye chuki au uwoga wa kufunikwa? Punguza chuki na uwoga rizki inapabgwa na Mungu.” Aliongeza kusema Mwijaku.
Kwenye albamu mpya ya Marioo iliyo na nyimbo 17 na iliyorekodiwa na lebo yake ya Bad Nation imetajwa kuwa tu sio toleo linguine bali ni mradi mkubwa unaoonyesha ukuaji, usanii na ushirikiano wa ajabu barani Afrika.
Marioo amewashirikisha wasanii wengine ikiwemo Jovial, Chino
Kidd, DJ Neptune na Poco Lee kati ya wasanii wengine.