Msanii wa muziki wa Kenya Bien amesifia jinsi alipokelewa nchini Tanzania alikokuwa ameenda kufanya shoo ya muziki iliyohusisha pia Sean Paul, Nandy na Ali Kiba.
Kwa mujibu wa Bien, mashabiki wa muziki kutoka nchini Tanzania hawakuondoka kwenye tafrija hiyo hadi wakati aliwatumbuiza mwendo wa saa kumi na mbili asubuhi.
Sifa za Bien kwa Watanzania zinajiri baada ya hali ya sintofahamu iliyotukia katika tafrija la Furaha City nchini Kenya ambapo kulishuhudiwa hali tete kufikia kiwango ambapo Diamond Platnumz wa Tanzania alikosa kuwaburudhisha mashabiki licha ya kutarajiwa zaidi.
Bien amesifia mapokezi aliyopewa na Watanzania kutoka uwanja wa ndege hadi kwenye jukwaa akielezea upendo waliokuwa nao.
“Nilipokelewa vizuri sana kuanzia uwanja wa ndege hadi kwenye jukwaa, wasee wa Tanzania walikuja wakaningija hadi saa kumi na mbili asubuhi nipande jukwaani.” Alisema Bien kwenye mahojiano na Ankali.
Bien aidha amesema kwamba ratiba ilichelewa kwa muda fulani akalazimika kuwaburudisha mashabiki mwendo wa saa kumi na mbili asubuhi alipopiga shoo baada ya Sean Paul, Ali Kiba na Nandy.
“Mafans walinipokea vizuri, walikaa mpaka asubuhi kuningojea , waliimba nyimbo zangu.
Ilikuwa baraka sana.” Alisema Bien.