Msanii wa ngoma za bongo tokea Tanzania Mbwana Yusuf Kilungi Maarufu Mbosso Khan ametoa shukrani kwa watu wote waliosaidia kufanikiasha matibabu yake pamoja waliomuombea dua.
Ameeleza kwamba tatizo hilo la moyo limekuwepo kwa muda mrefu tangu kuzaliwa kwake. Shughuli nzima ilichukua saa moja kukamilia upasuaji.
"Siku moja kabla ya jana ilikuwa saa 12 hadi mwisho wa 24 kwa hofu kubwa kwangu ambayo imeleta matokeo ya furaha na amani ya milele kwangu, familia yangu, na mashabiki wote wa muziki wangu. Nilipata fursa ya kutibiwa na madaktari bingwa wa moyo kutoka Misri (Misri 🇪🇬) pamoja na madaktari kutoka nyumbani hapa Tanzania ndani ya saa moja tu na kila kitu kilikamilika." alieleza Mbosso.
Mbosso alitoa shukrani zake za dhati kwa rais wa muungano wa Tanzania Samia Suluhu kwa kusaidia kwenye sekta ya afya jambo ambalo lilichangia Matibabu yake kuwa rahisi.
"Shukrani zangu za dhati ziwafikie popote Mulipo, Mheshimiwa Rais wa Tanzania. Shukrani kwa ajili ya mama! Chini ya utawala wako, uwezekano ambao niliongozwa kuamini hautawezekana hadi niende India. Shukrani kwa ajili ya mama! Kijana wako sasa yuko katika afya njema, na ninakuahidi kuwa nitashikamana nawe - mkoa kwa wilaya, vijiji kwa vitongoji ili kuhakikisha ninatangaza sifa za utendaji wako wa kazi." mwanamziki huyo alieleza.
Mwimbaji huyo awali aliwahi kufunguka kwamba alikuwa akisumbulilwa na matatizo ya moyo ambayo yalikuwa yakimukosesha amani na kumuacha na machungu ya kifua na mikono kutetemeka zaidi.
"Nina shida kubwa na moyo wangu, ila ninamshukuru Mungu kwamba naezafanya mazoezi na kuendelea kuwa sawa licha ya kwamba nafanya mazoezi mengi sana, mazoezi yenyewe yananiacha na machungu mengi. naweza kwenda kitandani ila niamuke nikiwa na machungu mengi zaidi hasa upande wa kushoto," alieleza.
Mbosso pia awali alikuwa amefichua kwamba matatizo hayo alikuwa ameyaweka kama siri ambayo alifichua tu kwa watu wa familia na bosi wake Diamond Platnamuz.
"Watu wachache sana walikuwa wanafahamu, mama yangu, wazazi wenzangu ambao nimepata nao watoto walikuwa wanafahamu ilikuwa huwezi kuwaficha lazima uwaambie ukweli maana chaweza tokea chochote na wakakusaidia. Bosi wangu anafahamu, Diamond nilimwambia yeye pekee yake," alieleza.
Mbosso alieleza kwamba aliambiwa na dakitari mwamba maradhi yake yalikuwa yanatokana na mishipa yake ilikuwa inazibwa na mafuta.