Msanii Alikiba
Ali Saleh Kiba almaarufu Alikiba ni msanii wa haiba na wa viwango vikubwa zaidi alizaliwa mnamo Novemba 29,1986 Kigoma Tanzania.
Alikiba pia hujiita jina la msimbo kama King Kiba anamiliki kituo cha King Music na kundi la Crown.Alikiba ni msanii ambaye amesifika sana katika taasinia ya mziki kwa muda mrefu sana.
Katika safari yake ya mziki Alikiba ni mwanamziki sifika na kando na kukuwa na uwezo wa kuporomosha magoma mazitomazito Alikiba pia ni mwigizaji,mwelekezaji na mwanasoka Hodari sana.
Baadhi ya vibao ambavyo Alikiba amewahi kuvitoa ni kama Mwana,Aje,Chekecha,Nakshi
Mrembo,Usiniseme miongoni mwa Vingine vingi.Alikiba ni msaani ambaye amevuma sana
kimziki na kutwaa zawadi na tuzo kochokocho ndani na nje ya Tanzania.
Ulipofika mwaka wa 2011 Alikiba alijipa mapumziko mafupi
kisha akarudi 2014 na kibao Mwana, kibao ambacho kilivuma na kupokelewa vyema na
mashabiki waliopendezwa na mahadhi yake kisauti na ujumbe mzito uliokuwa humo
ndani.
Jambo ambalo lilisababisha kutuzwa na kupokea zawadi kochokocho zaidi ya tuzo 5.
Katika orodha hiyo kibao chake cha AJE kilirodheshwa
nambari 3 katika nyimbo mia moja za Tanzania 2012-2022.
Alikiba alishirikiana na wasanii mbalimbali kuhakikisha kuwa
anaimarisha kipaji chake vyema na kuhakikisha kuwa kila kitu kinamuendea shwari
baadhi ya wasanii ambao aliwahi kushirikiana nao ni kama Partoranking,Sauti Soul, Mario
na Nyashisiki.
Alikiba kwa maisha yake kimziki amekuwa akipiga hatua ya
ufanisi muda baada ya muda, mnamo mwaka wa 2021 Kiba alizindua studio mpya na
kuwa na albamu ambayo aliita Mfalme mmoja ambayo ilikuwa imebeba nyimbo 16.
Mnamo mwaka wa 2022, Alikiba alishinda tuzo kadhaa tuzo
ikiwemo ya msanii bora, tuzo ya mwanavideo na mwanamziki bora nchini ni baadhi ya
tuzo ambazo nguli huyu kimziki amezitwaa na kuwa mfalme wa sanaa hii murwa.
Oktoba 3, 2024 Alikiba alizindua steshini yake mpya ya redio kwa jina Crown fm 92.1 , Kituo ambacho mawimbi yake yanashika Tanga, Pwani, Zanzibar, Dar es Salaam na Tanga.
Kwa hivyo bila shaka msanii Alikiba amekuwa kielelezo chema na mfano bora na hai wa kuigwa.
Kwa miezi ambayo imepita Alikiba amekuwa akishirikiana na msaani Darassa katika kolabo ya kucharaza vibao motomoto.
Alikiba anasalia kuwa miongoni mwa wasanii ambao malengo yao
yako juu na wanatumia mziki jinsi inavyostahili ili kuwalea wasanii chipukizi.