Safari ya msanii Masauti
Mohammed Ali Said almaarufu Masauti ni msanii wa Kenya aliyezaliwa
Mombasa Kenya.
Masauti ni msanii wa haiba ambaye anawakilisha kizazi cha leo
Katika mziki wa bongo. Msanii Masauti safari yake ya masomo ilikatizwa kutokana
na ukosefu wa karo kumwezesha kuendeleza masomo yako.
Katika umri wake akiwa mdogo Masauti alipenda sana
kuwasikiliza wasanii mbalimbali Pamoja na kujitungia nyimbo za kuimba. Mara si
mara alikuwa akizuru studio mbalimbali akiandamana na wasanii wenzake ili
kuvinjari mazingira ya studio.
Hapo ndipo Masauti alishikwa na uchu na ari ya kuanza kuimba
akawa akiijiita mswazi Masauti kijana mwenye kipaji cheupe tena mwenye ubunifu
mkubwa.
Itakumbukwa wazi kuwa masauti alianza kuimba akiwa na umri
wa miaka kumi na mitatu katika umri wake huo alikuwa kijana machachari tena mpwamu na mneni sana mbele ya halaiki.
Hatimaye Masauti aliweza kugura kutoka Mombasa kisha akaenda
Nairobi akiwa Nairobi aliendeleza injili ya usanii na kutambulika sana na watu
mbalimbali kisha akajisajili na msanii Teddy Josiah ambapo alikuja akatambuliwa
na Jalango mwaka wa 2019.
Jalango alimpokea masauti na kumpa nafasi siku moja katika Redio
huku akishirikiana na wasanii kama Khaligraph Jones wasanii waliomuandalia
mkeka wa makuzi na kumpa malezi bora kama msanii chipukukizi.
Masauti baada ya kuvalia magwanda rasmi ya mziki na kuwa msanii mwewnye malengo mapana baada
ya kuporomosha ngoma kali na kujiweka
katika viwango vikubwa alianza kuwa kipenzi
cha wengi wakiwemo pia mabinti waliommezea mate msanii Masauti.
Kuna siku tetesi
zilisema kuwa alikuwa kipenzi cha
msanii Nadia Mukami kutokana na ujio mpwa tena wenye nguzu aliokuwa nao
akachukua mtindo wake kisanaa na kujitambua sana.
Baadhi ya vibao ambavyo msanii masauti amevicharaza ni Ipepete,Sokote,Dondosha,liar,Inauma,Pepo na
Sare na kuonekana kidedeakatika taasinia hiyo ya mziki.
Msanii Masauti ni msanii mmojawapo ambaye anaiweka safu ya wasanii bora nchini kwa kuimba na kupanua mawanda ya mziki hadi ukanda wa afrika mashariki kwenye mitandao ya kijamii hasa ule wa instagram ana mashabiki elifu mia tatu tisini na wa tatu 393,000.