Mbwana Yusuf Kilungi alimaarufu Mbosso ni mwanamziki kutoka Tanzania alizaliwa Kibiti mwambao wa pwani mnamo Oktoba 3,1995.
Mbosso ni mtoto wa Yusufu Mbwana Kilungi na Khadija Salum Kikali wazazi ambao walikuwa wakifanya kazi za
kijungu jiko ili kujikimu kimaisha,baba alikuwa akifanya kazi ya Utingo huku
mama akifanya kazi ya ukulima.
Mbosso katika utoto
wake alikuwa mtoto mwerevu aliyependa masomo na kutunga nyimbo na kuziimba,aliazimia
kusoma zaidi ila kutokana na hali ngumu ya maisha na kipato kidogo cha familia
Mbosso alisoma hadi kidato cha nne.
Alipofika kidato cha nne na ikapatikana kuwa hamna hela za kumuwezesha
kuendelea na masomo aliwarai wazazi wake wampee kibali afuate nyota yake ya
talanta,Wazazi waliwazia ombi lake kisha wakamruhusu afuate azima yake kama msanii.
Katika safari yake ya Maisha Mbosso alionekana kidedea na mchangamfu
sana ka kila hatua aliopiga ilizaa matunda.
Baada ya Mbosso kuwaza sana ni wapi atakapoanzisha maisha
yake upya aliamua kugura nyumbani na kuenda Dar salaam kuenda kutingiza kibiriti kuona kama ndani
mna njiti.
Alipofika Dar es Saalam
alikumbana na ugumu wa hali ya maisha akawa na hali tete kimawazo alipokuwa
katika shughuli zake za hapa na pale alikutana na mkubwa na wanawe ambaye alimshika
mkono na kumshirikisha katika bendi iliyovuma sana ya Yamoto Bendi.
Akijiunga na bendi hiyo ya Yamoto bendi ambayo
iliwashirikisha vijana wenzake wenye vipawa angavu kama chake waliweza kuimba
nyimbo ambazo zilikuja zikavutia mashabiki na kuwa kipenzi cha wengi nchini Tanzania
na ukanda wa Afrika mashariki kwa jumla.
Mbosso alikuwa na wasanii wenzake kwa jina Aslay ,Beka Flavour na Enock Bella waliovuma 2018 na kuwa mahiri wakubwa
na kuonyesha ushuja na ubunifu wa hali ya juu sana.
Baadhi ya Vibao ambavyo mbosso alivicharaza baada ya bendi
yao maalum Yamoto bendi kuvunjika na hatimaye akajisajili na lebo ya Wasafi rekodi Sambapo aling’ara zaidi baadhi ya Vibao
alivyovicharaza ni Nadekezwa,Hodari,Watakubali miongoni mwa vingine vingi zaidi.