Mwanamuziki Tajika nchini Tanzania Diamond Platinumz akizungumza kuhusu Trace Awards ambazo zitakuwa zikifanyika nchini Tanzania siku ya Jumatano, alionyesha imani hasa kwa taifa kwa kufikia kiwango hicho.
Alipongeza viongozi walioko mamlakani hasa mama Samia Suluhu na kiongozi wa Zanzibar Hassan Ali Mwinyi kwa kazi nzuri ya kukuza Tanzania ili kufikia katika kiwango cha kimataifa.
"Kwanza kabisa nipongeze nchi kwa unyenyekevu na utulivu wake uliopelekea watu kama Trace kuona kuja kufanya, nipongeze nchi ya muungano wa Tanzania rais Samia Suluhu Hassan. lakini pia nimpongeze rais wa mapinduzi ya serikali ya Zanzibar Dkt Hassan Ali Mwinyi kwa kazi nzuri anayofanya. Hawa wote kwa utoaji wao wa shughuli hizi wamesababisha kitu kama Trace kuja kufanyika hapa. Maaana wao wanaangalia mazingira mazuri, amani na upendo wa watu," alisema Diamond
Nyota huyo wa muziki wa bongo nchini kando na kuwapongeza viongozi pia alionyesha imani yake, kwamba wao kama wasanii watanufaika pakubwa.
Alisema ana imani kwamba wao kama wasanii wa Tanzania ambao watakuwa wenyeji watajitahidi, akiwataka wenzake kuhakikisha kwamba wamejipanga vya kutosha.
Wakati huo pia aliweka imani kwamba wasanii wa Tanzania watajitokeza kwa wingi maana hafla hiyo iko nyumbani.
"Nafasi hii ni ya kukuza siyo tu sana. kuna nafasi ya wasanii wengi kuperfom Tanzania kwa sababu inafanyika nyumbani kwetu. tuna mengi ya kuyafanya na naamini wanamziki wa Tanzania tumejiandaa kwelikweli kuhakikisha kwamba hatuwaangushi. Tutawaakilisha vyema na kutangaza mziki wetu. hili onesho ni kubwa linatazamwa na watu wengi duniani," rais huyo wa wasafi alifafanua.
Diamond pia alionesha imani kwamba ni wakati sasa wa taifa la Tanzania kutangaza utali wake kupitia fursa hii ambayo wamepata kwa mara ya kwanza.
"Hili zoezi linatangaza utali kwa ukubwa sana. Nchi yetu sasa inatajwa sio tu Africa lakini ulimwengu mzima," alieleza Platinumz
Msanii huyo ameonesha imani kwamba wakati tamasha hilo litakapokamilika litakuwa limeacha histora kwa nchi ya Tanzania .
Wakati huo pia amempongeza kiongozi wa Zanzibar kwa kufungua mkutano kukaribisha wageni ambao tayari wamewasili leo Jumanne 25.
Tuzo za Trace Awards zinaonyesha utajiri na ubora wa muziki wa Afro kupitia aina kama Afrobeat, dancehall, hip-hop, Afropop, mbalax, amapiano, zouk, kizomba, genge, coupé-décalé, bongo flava, soukous, injili, rap, raï, kompa, R&B, na rumba.
Wasanii kutoka nchi zaidi ya 30 barani Afrika, Amerika ya Kusini, Caribbean, Bahari ya Hindi, na Ulaya wanashindana katika makundi 24.