John Philip Ouma alimaarufu msanii Madini Classic ni msanii wa
Bongo Mkenya mzaliwa wa Kisumu.
Alizaliwa mnamo Desemba 2,1994 katika gatuzi la Kisumu mkoa
wa Nyanza Japo aligura na Kwenda nchi ya Tanzania wakati ambapo kipaji chake
cha usanii kilichipuka.
Baada ya muda Madini alirudi nchini Kenya na kuka upande wa
Pwani,alianza safari yake ya usanii akiwa mdogo alipokuwa akijifunza kuimba
miziki aina ya bongo.
Katika hali yake ya udogo na ujana Madini alikuwa akiimba na kurekodi nyimbo kadhaa ila alikosa mtaji wa kurekodi video akawa ametulia chini ya zulia akisubiri hali imwendee nyema kihela.
Madini classic alipagazwa jina MADINI kutoka kwa babu
yake aliyekuwa anafanya kazi nchii ya
Tanzania ambaye alikuwa mchimba migodi mahiri na madini kule Taifa la Tanzania.
Katika safari yake ya muziki madini classic alivicharaza
vibao kadha ambavyo vilimkweza na kumuweka katika safu ya wasanii bora ukanda
wa Afrika Mashariki na Kati hadi upande wa janga la Sahara na baadhi ya sehemu
za Mto Limpopo.
Baadhi ya Vibao ambavyo Madini ameviachilia ni Nitalewa,Taratibu,Goma,Toto
la Kanairo,Bingo Bango,Tawire miongoni mwa vibao mbalimbali ambavyo
vilihanikiza na kuteka anga kwa mirindimo ya kipekee.
Katika mahojiano na kituo cha Habari cha Mpasho Madini
aliwahi sema na kusadiki kuwa mara
nyingi yeye huwa hapendi kuishi maisha ya bandia ili ifahamike na watu kuwa
hali yake ya Maisha i sawa kumbe la.
Madini alielelezea kuwa katika safari yake ya muziki na
maisha yake kwa jumla hajawahi kuazia kujihusisha na maisha ya kughushi katika hali
halisi ya hapa duniani yeye hukiri na kususia
lile ambalo anahisi haliko sawa ila si
kufurahisha umma jinsi wasani wengi kwa
asilimia kubwa wanavyofanya.
Madini kutokana na mujibu wa maelezo yake alisema kuwa mara
nyingi wasanii wengi huwa na hulka ya kutaka
sifa na majitapo na kutaka kujulikanaa hivyo kuishia kufanya vitu ambavyo ni kinaya cha kuogofya na uhalisia
wa maisha yao.
Kulingana na kujitambua huko kwa Madini ndiko kumempa jina kubwa jina ambalo limejulikana na kupata umaarufu wa
hali ya juu sana.
Msanii Madini Classic unaposikiliza vibao vyake utagundua kuwa ni msanii ambaye amezamia kwa lugha ya Kiswahili sanifu yeye ni msanii ambaye ni mtunzi mzuri wa Mashairi ambayo huwa na ujumbe kwa jamii katika viwango vyote si elimu, kilimo ,biashara,siasa na mapenzi ujumbe huwa huwa umekolea sana.