
Mwanamuziki Dully Sykes kutoka nchini Tanzania sasa anadai kwamba ni yeye aliyegundua kipaji cha msani maarufu wa bongo fleva Alikiba ambaye pia ni mzaliwa wa taifa la Tanzania.
Dully alikuwa anazungumza haya kwenye mahojiano na mwanahabari huku akimusifia Alikiba kama msani mkubwa sana na ambaye amekubalika kimataifa.
Msanii Dully alifichua kwamba aliwahi kugharamia gharama yote ya muziki wa Alikiba pamoja na kumusaidia hela ya kutolea video pamoja na nauli ya kwenda na kurudi.
"Nimepata kolabo kubwa kutokaka kwa Alikiba. Alikiba ni msani mkubwa sana, ni msanii wa kimataifa, alinipa kolabo na akashughulikia video. Yeye alishughulikia promotion," alisema Dully.
"Mimi si shemeji yake labda nimempa dada yangu au nimemuoa dada yake, ni kwa sababu nimeishi naye vizuri na nimegundua kipaji chake. Nilimbeba nikamueka kwenye gari nikampeleka situdio nikampa pesa ya nauli ya kurudi. Nikawa na yeye karibu, nikampa mawazo.,"aleindelea mwanamziki huyo wa Tanzania.
Wakati akizungumza pia ameweka wazi kwamba katika maisha kila mtu anamhitaji mwingine ili kusonga hatua katika maisha. Ameongeza akieleza kwamba mwanadamu anahitaji kuwa na msimgi mwema na watu ili kujikimu hasa wakati anapokumbwa na masaibu.
"Katika maisha lazima tutengeneze vizazi na lazima tuwe na mtaji watu, tutengeneze izi misingi kwa ajili yao. Utengeneze watu, kesho na kesho kutwa wanakuja kukusaidia. Mimi nimesaidiwa na watu sio eti mimi naweza kuimba sana au mimi sina mawazo lakini naweza kustahimili kwa sababu napata msaada wa haraka sana," alisisitiza.
Dully pia alifichuwa kwamba kutokana na kujitolea kuwasaidia watu pia anapata msaada huku akimurejelea baba yake mzazi wa Mario ambaye aliwahi kumusaidia baada ya kumusaidia mtoto wake.
"Mario huyu hapa nimefanya naye kazi, kanisaidia baba yake, kwa ajili gani? Mwanawe nimeishi naye vizuri amekuwa katika mikono yangu. Kwa hivyo misingi lazima tutengeneze kabla hakujachacha," alifichua Dully.
Dully Sykes ambaye jina lake halisi ni Abdul Sykes alizaliwa tarehe 4 Desemba 1980. Ni mwanamuziki wa Bongo Flava kutoka Tanzania, mtunzi wa nyimbo na mtayarishaji wa rekodi.
Dully Sykes ana sifa kubwa ya kuinua wasani wenye majina makubwa katika tasnia ya muziki ikiwa ni pamoja na Marioo, Shetta na marehemu Pancho latino. Mwaka 2022, alishirikisha mwimbaji wa Tanzania, Kusah katika kibao chake cha 'Do Do.'