logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wazazi wa Kiume msikatae watoto - Jay Melody

Melody amewapa wasia wazazi wa kiume wernye tambia ya kuwaacha watoto na kudai sio wao.

image
na Japheth Nyongesa

Mastaa wako17 March 2025 - 11:57

Muhtasari


  • Amesisitiza kwamba ni vyema kuonesha upendo kwa mwanao na akifanikiwa kwa siku za baadaye huenda akarejesha mkono.
  • Mwanamziki huyo wa bongo pia amefanya kolabo kadhaa na wasanii wakubwa nchini Tanzania.

Jay Melody
Mwanamziki Sharif Said Juma maarufu Jay Melody kwenye tasnia ya muziki amewapa wasia wazazi wa kiume wenye tambia ya kuwaacha watoto na kudai sio wao.

Msanii Melody aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwaonea huruma wazazi wanaowatenga wanao hasa uja uzito unapotokea bila kupangwa.

Amesisitiza kwamba ni vyema kuonesha upendo kwa mwanao na akifanikiwa kwa siku za baadaye huenda akarejesha mkono tofauti kabisa na iwapo wataweatengwa wanao.

"Kama umepata mtoto, iwe hukupenga au vyovyote vile, usifanye kosa la kutokumulea huyo mtoto. Baadae mtoto akiwa na maisha yake utaleta lawama na yeye hatokujali kama ulivyofanya. wazee tulee watoto wetu. watoto ni baraka," alindika mwanamziki Melody.

Jay Melody ambaye kwa sasa Machi 2025 ana umri wa miaka 28, kando na kuwa mwimbaji ni mwandishi wa nyimbo. Ameimbaa vibao kadhaa vikiwemo, Nakupenda, Sawa, Wa pekee yangu, Nitasema, miongoni mwa vibao vingine.

Mwaka 2016 ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Jay Melody kuingia katika tasnia ya muziki alipojiunga na chuo kikuu cha Tanzania House of Talent (THT).
Baada ya mwaka mmoja wa kujifunza muziki Jay Melody hatimaye alisainiwa na Epic Records Tanzania moja ya lebo kubwa za rekodi nchini zinazomilikiwa na Genius Ruge Mutahaba na kuwaachiwa wimbo wake wa kwanza unaokwenda kwa jina 'Goroka'

Mwanamziki huyo wa bongo pia amefanya kolabo kadhaa na wasanii wakubwa nchini Tanzania akiwemo kiongozi wa Wasafi Diamond Platinumz.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved