Kwenye mazungumzo na wanahabari amekiri kwamba yeye alianza mipango ya kufunga ndoa na mrembo huyo pindi tu baada ya kukutana ila Fahymah hakuwa tayari kwani alihofia kwamba angali mdogo kiumri.
"Mwaka wa kwanza nimeanza naye, nilikuwa na moto sana. Ata sijatoka, kwetu wajatoka ivo, nishaanza kupanga mipango. Ila nakwambia akakataa akisema mimi bado mdogo. Nikamwambia vipi bwana nioe akasema apana mimi bado mdogo, ngoja kwanza subiri nikamwambia sawa," alifichua Rayvanny.
"Nikamwambia sawa, vitu vitakuwa vizuri acha tungoje muda. Nafikiria kwa sasa hivi niko tayari na mwenyewe pia amefurahi kwa hili. Mwanamke kuolewa ni furaha. Alafu pia marafiki, unapoona watu wake wengi wa pembeni, marafiki wake wengi unajua.. bwana akuoe. Ila mimi siowi kwamba nalazimishwa. Naoa kwa sababu mimi nataka," aliweka wazi.
Msanii Rayvanny amemsifia mrembo wake Fahymah huku akimtaja kama mwanamke wa kipekee na tabia za kupendeza mwenye akili ya kutatua mambo kwa njia nzuri. Ameeleza kwamba ni mwanadada ambaye hana hasira na anajua kutatua mambo.
"Fahymah ni mwanamke ambaye ni mvumilivu, ni mwanamke ambaye anaweza kukuletea heshima. Akiwa na asira siyo mwanamke ambaye anaweza tenda matukio ya kukuudhi. Kwa hivyo ukimpoteza mtu wa namna hiyo... Unajua unapomfanyia mwanamke vitimbwi, anapata mshauri na anakutana na vishawishi vingi," alieleza Rayvanny.
Mwanamuziki huyo aliweka wazi kwamba hayuko tayari kumpoteza Fahymah kwani ni chaguo lake na yuko na kila sababu za kumheshimu.
'Mtu ambaye anaweza akawa upande wako akakuletea heshima. anahakikisha hauchafuki kwenye umati mheshimu. Sio watu wote wanaweza hilo," alisema mwanamuziki huyo wa lebo ya Next Leval Music.
Fahyvanny ambaye ni mpenzi wa mwimbaji huyo maarufu wa Tanzania ni mzaliwa wa nchi hiyo ya Tanzania. Yeye na Rayvanny hawajawahi kuachana rasmi tangu kuanza mahusiano yao.