logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Profesa Jay afichua kufilisika baada ya kuuza mali zake ili kugharamia matibabu

Profesa Jay kutokea nchini Tanzania amefichua kwamba alilazimika kuuza mali zake ili kugharamia matibabu.

image
na Japheth Nyongesa

Mastaa wako24 March 2025 - 16:56

Muhtasari


  • Wakati huo amewapa mawaidha watu na kuwaomba kuchunguza hali zao za afya mara kwa mara.
  • Profesa Jay ni mmoja wa waanzilishi au wasanii wa mwanzo kabisa katika muziki wa hip hop wa Tanzania.

Profesa Jay
Mwanasiasa na mwanamziki maarufu wa hip hop, Joseph Leonard Haule anayejulikana kwa kwa jina la usani kama Profesa Jay kutokea nchini Tanzania amefichua kwamba alilazimika kuuza mali zake ili kugharamia matibabu.

Profesa ambaye amekuwa akiugua na wakati mmjoa kukaa hospitalini karibu mwaka mzima alikua akizungumzia changamoto zinazokuja na magonjwa yasio ya kuambukizana.

Mwanamziki huyo wa zamani alikua akizungumza haya kupitia mahojiano na wanahabari ambapo alifichua changamoto alizokumbana nazo wakati wa kugharamia matibabu.

"Haya magonjwa mimi nimeumwa na najua gharama zake ni kubwa, imenifilisisha kabisa kwa sababu ya kujitibu. Niliuza mali zangu kwa ajili ya kujitibu. Hali ilikuwa mbaya sana na gharama ni kubwa sana. Dalisisi wakati mmoja ni laki tatu na unafaa kwenda mara tatu kwa wiki, hizo ni laki tisa," alifichua Jay.

Mwanamziki huyo ameeleza kwamba Gharama ya matibabu kwa magonjwa ni makubwa ni changamoto kubwa sana kwa watu ambao ni wa kiwamngo cha chini katika maisha.

Msanii huyo pia ameeleza kwamba wamelazimika kufufua upya wakfu wa Profesa Jay Foundation ili kusaidia watu wasiojiweza kuafikia matibabu kwa magojwa hatari na yasioambukiza.

"Mama nitilie au watu wa bodaboda hawawezi kumudu matibabu, kila mwezi ni karibu milioni moja na laki mbili [za kitanzania] inakua ni hela nyingi sana kwa mtanzania wa kawaida. Ndo maana nikaona niwashike mkono wapate mafunzo, wakapimwe, na ikigunduliwe mapema wapate tiba," alisema mwanasiasa huyo.

Wakati huo amewapa mawaidha watu na kuwaomba kuchunguza hali zao za afya mara kwa mara ili kugundua magonjwa mapema na huenda ikawa rahisi kutibiwa na kupona.

"Watu wajikinge, wakapiwe na utaratibu wake ukingundua mapem, Kuweni na tabia ya kuangalia afya mapema. Ukiwa na tabia ya kupima mara kwa mara unaweza kujikuta una magojwa katika hali ya mwanzo utapewa vidonge tu na utapona. lakini ikiwa kwenge steji 4, 5 inakuwa hali mbaya sana na wengi wanapoteza maisha," alileza.

"Magonjwa yasioambukiza kama vile figo, saratani, Kisukari, Pressure, ni gharama kubwa alafu hayana usaidizi. Hakuna NGOs za kimataifa ambazo zinashughulikia magonjwa kama hayo," alieleza zaidi mwanamziki huyo wa zamani.

Profesa Jay ni mmoja wa waanzilishi au wasanii wa mwanzo kabisa katika muziki wa hip hop wa Tanzania.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved