logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Safari na usuli wa msanii Nyashiski

Msanii Nyamari Ongegu alimaarufu Nyashisiki ni msanii wa miziki aina ya bongo na hip hop mzaliwa wa Kisii Kenya.

image
na Evans Omoto

Mastaa wako26 March 2025 - 15:04

Muhtasari


  • Nyashisiki alizaliwa mnamo Aprili 8,1984 na msanii ambaye amekuwa kwa taasinia ya uanahabari tangu mwaka wa 1999 hadi leo akihesabu jumla ya miaka 24 akiwa katika taasinia.
  • Alipokuwa katika shule ya upili aliweza kutoa kibao kwa jina freek mwaka wa2002 chini ya lebo kali sana ya Ogopa DJ kilichofuatwa na Maniax Athem vibao ambavyo vilitamba sana.

Msanii Nyamari Ongegu alimaarufu Nyashisiki ni msanii wa miziki  aina ya bongo na hip hop mzaliwa wa Kisii Kenya.

Nyashisiki alizaliwa mnamo Aprili 8,1984 na msanii ambaye amekuwa kwa taasinia ya uanahabari tangu mwaka wa 1999 hadi leo akihesabu jumla ya miaka 24 akiwa katika taasinia.

Msanii Nyashisiki amekua ni msanii wa haiba tena mwenye viwango vya juu sana katika sanaa hii ili kuweza kustahimili mawimbi ya kimziki,Nyota yake kimziki ilianza kung'ara wakati ambapo alipokuwa katika shule ya upili  ambapo aliweza kukutana na wasanii Robert Manyasa na Collins Majale miaka ya zamani 1999 alipokuwa katika shule ya upili ya Nairobi.

Alipokuwa katika shule ya upili aliweza kutoa kibao kwa jina freek mwaka wa 2002 chini ya lebo kali sana ya Ogopa DJ kilichofuatwa na Maniax Athem vibao ambavyo vilitamba sana.

Baada ya hapo msanii Nyashisikii alianza kuvuna na kujulikana sana na mashabiki waliompennda na kumwona kama msanii wa haiba ya juu sana mnamo mwaka wa 2004.

Mwaka 2009 Nyashisiki alianza kuimba kama msanii wa kujitegemea na kuonyesha wazi kipaji chake kama msanii mwenye uwezo wa kutunga na kuimba mashairi mazuri tena ya kupendeza .

Baadhi ya vibao ambavyo msanii huyo wakipekee amevicharaza ni kama ifuatavyo perfect design mwaka 2023,bebi bebi,Mungu pekee,Malaika,Free,Hayawani,Hapo tu, lifti  me up, utazoea miongoni mwa vingine.

Katika safari yake Nyashisiki alipokea tuzo kadhaa kama vile Pulse MUSIC Video Awards mwaka wa 2016 ,best African Act mwaka 2017 na mwaka wa 2018,mwaka wa 2022 alipewa tuzo kama msanii bora  wa kiume wa Afrika Mashariki miongoni mwa tuzo nyingine nyingi.

Hata hivyo msanii Nyashiskii kutokana na kujituma kwake na kuonyesha ari kuu ya kuweza kuimba na kutunga nyimbo zenye hadhi kuu ni kuwa anasalia kuwa msanii bora tena wa haiba kuu katika ulingo wa wasanii bora katika Afrika Mashariki na kuwa msanii bora katika taifa la KENYA.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved