Macvoice ameonekana kwenye video tofauti akitumbuiza sehemu duni sana jambo ambalo limewafanya mashabiki wake na mashabiki wa muziki wa bongo kwa ujumla kutilia shaka utendakazi wa lebo inayommiliki.
Rayvanny ambaye ni rais wa lebo hiyo ya Next Leval Music kwenye mahojiano na mwanahabari ameeleza kwamba kwa upande wake hajui kilichomfika mwanamuziki wake.
Akizungumza amejitenga na madai kwamba alimutoa Macvoice kutoka kwenye lebo hiyo. Alidinda kueleza kwa kina kususu sakata hilo akiahidi kutoa taarifa kamili baada ya kamati nzima ya lebo kukua na kikao.
"Nafikiri sio muda sahihi kuzungumza hili swala, mwenyewe nimeona kama ambavyo umeona wewe, nikikaa na kamati nzima ya lebo nafikiria pia wao watakua na neno la kusema. Rayvanny ni mkurugenzi lakini kuna wale ambao pia wana la kusema," alieleza.
Kiongozi huyo wa Next Leval Music pia amewataka watu kutoangazia tu changamoto lakini pia wazungumze mambo yanapokwenda vizuri na pia kutoa kongole.
"Lakini niseme kitu kingine kwamba wakati mwingine kuna kuchanganyikiwa kwa kile tunachokiona mtandaoni. Unajua vitu vibaya ndivyo vinasambaa sana kuliko vitu vizuri,' alikariri.
"Lakini nafikiri kwamba vijana wanafaa kusaidiwa zaidi, wasukumwe wafike mbali. Vijana wanapitia vitu vingi sana. Siongelei Macvoice pekee ni kwa wote. Ingekuwa msani ametumbuiza kwenye uwanja uliojaa watu hawatazungumzia hilo. Ila wakiona kama kuna changamoto hivyo ndivyo vitu ambavyo wanapenda kuviongelelea," Raivanny alisema.
Mwanamziki huyo maarufu katika ukanda wa Afrkia mashariki amesisitiza kwamba wakati sahihi utafika na ataeleza kwa kina kuhusu mwanamziki wake Marcvoice.
"Nitatoa ya Lebo nzima kama mkurugenzi ila si kwa sasa. Nimeona mlivyoona nyinnyi lakini naahidi tutalizungumzia," alisema.