
Zuchu kwenye mahojiano na mwanahabari ameweka wazi kwamba anampenda Diamond na hayuko tarari kumpoteza akiahidi kumung'ang'ania mpaka mwisho.
Wakati huo pia ameeleza kwamba ana imani kwamba Diamond anampenda na pia anamung'ang'ania.
Nasikia raha kushinda nikimng'ang'ania mpenzi wangu. Sidhani kama kuna mwanamke anaeza hilo, kama yuko sidhani. Nasikia raha sana kumng'ang'ania. Mimi ni king'ang'anizi na nitamung'ang'ania mpaka mwisho. Raha ya Kung'ang'ania siku zote nasema ni wewe pia ung'ang'aniwe. Sio kung'ania usipong'ang'aniwa. Mimi na Diamond tunang'ang'aniana, " alieleza
Mwanadada huyo pia anamtaka mrembo yeyote anayejiamini kwamba Diamond ni mpenzi wake ajitokeze hadharani wakutane.
"Kama wewe ni mwanamke unajiamini kwamba Diamond ni mwanaume wako jitokeze tuone," aliweka wazi mwanamuziki huyo wa kibao cha Napambana.
Zuchu ambaye amekuwa mpenzi wa mwanamuzuiki Diamond kwa muda sasa ni mwanamuziki wa lebo ya Wasafi ambayo inamilikiwa na huyo mpenzi wake.
Wanamuziki hao wawili waliweka wazi mahusiano yao ya kimapenzi mwezi novemba 2022 baada ya uvumi huo kuwepo kwa muda mrefu kabla ya hapo.
Mwanamuziki Zuchu alianza kuvuma na kuteka anga za utumbuizaji baada ya kujiunga na wasafi, jambo ambalo linatajwa kwamba zilikuwa juhudi za mama yake mzazi kuwaunganisha na Diamond ili amshike mkono.
Licha ya kwamba Zuchu ana mapenzi ya dhati mwa rais huyo wa Wasafi, wafwasi wao wanabaki na maswali chungu nzima iwapo atafaulu kumutuliza Diamond kwani ni mmoja kati ya wanamuziki ambao wamefaulu kupenndwa na wanawake wengi.
Baadhi ya wanawake warembo na maarufua ambao walijaribu kumkaba Diamond ila hawakufaulu ni pamoja na Hamisa Mobeto, Wema Sepetu, Zari Hassan na Tanasha Donna.