Akothee awashauri wazazi kufanya mzaha na watoto wao

Amesema uhusiano mzuri kati ya wazazi na watoto unaweza kuwafanya wawe wazi juu ya maisha yao.

Muhtasari

•Akothee anadai kuwa uhusiano mzuri kati ya wazazi na watoto wao unaweza kuwafanya watoto kuwa wazi juu ya maisha yao ya faragha  bila hofu yoyote

•Anatamani ikiwa mama yake angeweza pia kufanya utani naye kama vile anavyofanya na watoto wake kila wakati.

Mwanamuziki mashuhuri Esther Akoth almaarufu Akothee ​​amesihi wazazi kuwa huru na watoto wao wakati wote na ikiwezekana wafanye  utani nao ili kuimarisha uhusiano kwenye familia.

Mama huyo wa watoto watano anadai kuwa uhusiano mzuri kati ya wazazi na watoto wao unaweza kuwafanya watoto kuwa wazi juu ya maisha yao ya faragha  bila hofu yoyote.

''Watoto wangu wanapenda kutaniana na  wanacheza sana'' Akothee alisema.

Akothe ​​anatamani ikiwa mama yake angeweza pia kufanya utani naye kama vile anavyofanya na watoto wake kila wakati.

''Mama yangu hata  hawezi kupiga selfie nami'' Aliongeza.

Akothee
Akothee
Image: HISANI

Ujumbe huo kupitia ukurasa wake wa Instragram iliibua hisia tofauti kutoka kwa wafuasi wake ambao baadhi yao hawana uhuru wa kutaniana katika familia zao.

 Mmoja wa shabiki wake kwa  ukurasa wake wa Instagram kwa  jina  Nyambura148 alisema  ''kwanini mama yangu hawezi kuwa kama wewe''

Wengine pia kupitia mchango wao kwenye ukurasa huo  walionekana  kukuwa na maswali ambazo wangelitaka kuwauliza wazazi wao kuhusu kizuizi cha uhuru wao wa kufanya mzaha nao.

Christine maina6 alikuwa na haya ya kusema''mama yangu anafaa kunieleza  kwa nini hajawahi kunipa nafasi ya kufanya utani naye hivi''

Hivyo vijana wengi wametamani kuwa na wakati mzuri na wazazi wao ili kupunguza matukio ya hofu kwa baadhi ya Vijana dhidi ya  wazazi wao ambao ni wakali mno.

''Napenda jinsi mnafurahia maisha nawapenda sana''Macharia3693 ambaye ni shabiki alidokeza.