Colonel Mustafa aomba msaada wa kumshugulikia mama yake anayeugua saratani

Alibainisha kuwa shida yake kubwa kwa sasa ni matibabu ya gharama kubwa ya mama yake

Muhtasari

•Mustapha alitaja kuwa anahitaji kazi au mtaji kuanzisha biashara ili aweze kuweka chakula mezani na kulipa bili kadhaa.

•"Mziki haijakuwa ikifanya vizui, kila nikitoa muziki inakataa."aliongeza.

Msanii mkongwe kutoka Ogopa Djs, Coonel Mustafa
Msanii mkongwe kutoka Ogopa Djs, Coonel Mustafa
Image: Colonel Mustafa (Instagram)

Mwanamuziki nguli wa Kenya Colonel Mustapha ameomba msaada kutoka kwa watu wema ili kuweza kumshughulikia mama yake ambaye ni mgonjwa.

Katika mahojiano na Eve Mungai, Mustapha alitaja kuwa anahitaji kazi au mtaji kuanzisha biashara ili aweze kuweka chakula mezani na kulipa bili kadhaa.

Alibainisha kuwa shida yake kubwa kwa sasa ni matibabu ya gharama kubwa ya mama yake kwani anaugua saratani.

“Sifikirii kufanya muziki; Nahitaji kazi, kitu ninachoweza kufanya, ili kujisaidia. Ninaweza kusimamia klabu, naweza kufungua duka na pia nina duka ambalo liko karibu kufungwa kwa sababu ‘nimekula hisa yote,”.

“Kwa sasa hatujasajili namba ya till lakini bado wanaweza kutuma kwa namba yangu 0722803924 –Daud Mustaspha.

"Nikipata njia za kuongeza bidhaa naweza kuendelea kuuza duka," alisema.

Aliendelea kufichua kuwa amefanya kazi za ‘Mjengo’ kwa takribani mwaka mmoja na amekuwa akifanya kwa siri kutokana na hadhi yake katika jamii.

Alikiri kuwa kazi yake ya muziki imekuwa haifanyi vizuri na kila anapotoa wimbo hauvumii na kuongeza kuwa huwa hapati mapato kutokana na nyimbo zake za awali.

"Mziki haijakuwa ikifanya vizui, kila nikitoa muziki inakataa."aliongeza.

Kulingana na Mustapha, dhiki zake zilianza 2020, wakati wa Corona.

"Ilianzia kati ya Nairobi Diaries ikashikana na corona ambayo iliua kila kitu lakini najaribu sana. Nilichukua kazi ya mjengo kumsaidia mama kwa sababu mimi bila yeye sijui."

"Kuna wakati nilijaribu kutafuta msaada lakini marafiki walipiga screenshot na kutuma, lakini nilifanya mengi kukomesha hilo."

Rapa huyo alieleza zaidi kuwa mama yake amekuwa akiugua kwa muda na huwa anaingia na kutoka Hospitalini kwa matibabu ya Kemotherapy.