Michelle Ntalami azungumzia hali ya mahusiano baada ya kuokoka

"Sijui ni mara ngapi nitahitaji kufafanua hili. Nimekutana na wanaume hapo awali" alisema.

Muhtasari

•Michelle alisema kwamba yuko tayari tu kutoa jibu wazi juu ya upendeleo wake kuhusu swala la uchumba tu wakati ambao ataonyeshwa na Mungu.

• Ntalami alisema kuwa aliwahi kuwa katika mahusiano na wanaume na kwamba alionyeshwa na Mungu kwamba wanaume walikuwa sehemu ya maisha wake wenye uchungu.

Michelle Ntallami
Michelle Ntallami
Image: instagram/michelle

Mkurugenzi Mtendaji wa Marini Naturals Michelle Ntalami ambaye hivi majuzi alitangaza kuokoka ametangaza waziwazi nia yake ya kushikamana na Mungu baada ya wito wake.

Katika mahojiano ya hivi majuzi,  Ntalami alishiriki maarifa kuhusu mapendeleo yake inapokuja suala la uchumba.

Hapo awali, Ntalami alisemekana kuwa anachumbiana na Makena Njeri kwani mara nyingi walitumia muda pamoja na kutangaza waziwazi kuwa wanapendana.

Ntalami hakuweza tena kukwepa swali juu ya upendeleo wake linapokuja suala la kuchumbiana sasa kwa vile ameokoka.

Pamoja na mwonekano wake wa kuvutia, Ntalami alisema kuwa aliwahi kuwa katika mahusiano na wanaume na kwamba alionyeshwa na Mungu kwamba wanaume walikuwa sehemu ya maisha yake yenye uchungu.

"Sijui ni mara ngapi nitahitaji kufafanua hili. Nimekutana na wanaume hapo awali katika maisha yangu na pia walikuwa sehemu ya maisha yangu ya uchungu ambao Mungu alinionyesha.

 Ni kwamba labda baadhi ya uhusiano wangu ulikuwa nje kwenye vyombo vya habari.

"Kabla ya hapo, nilikuwa nikichumbiana na wanaume. Wakati huo utambulisho wangu ulikuwa androsexual, neno ambalo linamaanisha mtu anavutiwa na wanaume au nguvu za kiume. Siku zote nahisi kama kuna dhana kwamba sichumbii  wanaume kabisa,” Michelle alifafanua.

Michelle alisema kwamba yuko tayari tu kutoa jibu wazi juu ya upendeleo wake kuhusu swala la uchumba tu wakati ambao ataonyeshwa na Mungu.

Mwezi uliopita, Michelle Ntalami alishiriki na mashabiki wake mabadiliko mapya katika maisha yake baada ya wito wa Mungu.

Michelle alitangaza hadharani upande wake mpya, akitaja kwamba alikuwa amezungukwa na marafiki wa mbaya kati yake.