Muigizaji Maria hatimaye azungumza baada ya kushirikishwa kwenye kipindi cha Sultana

Maria yuko kwenye televisheni tena, jambo ambalo limewaacha wengi wakiwa na furaha.

Muhtasari

•Lulu Hassan ambaye ndiye anamiliki na kuelekeza shoo hiyo alitangaza kuwa Maria angehusika tena kwenye shoo ya sultana ambayo wengi wamekuwa wakisubiri.

YASMEEN SAIEDI
Image: KWA HISANI

Ikiwa wewe ni mtumizi wa mitandao ya kijamii wa mara kwa mara lazima umekutana na muigizaji Yasmeen Said kwa wakati fulani.

Wengi wanamfahamu kwa jina la kisanii "Maria Wa kitaa" au Maria kutoka citizen tv.

Alipata umaarufu baada ya kuwa muigizaji mkuu katika kipindi cha Maria kilichokuwa kikipeperushwa kwenye runinga ya citizen takriban mwaka mmoja uliopita.

Baada ya kipindi hicho kuisha na kipindi cha sultana kuchukua nafasi yake, ilibidi wapakie na kuondoka jambo ambalo liliwaacha wengi wakiuliza kuhusu baada ya kukosekana tena kwenye skrini zetu.

Hivi majuzi, Lulu Hassan ambaye ndiye anamiliki na kuelekeza shoo hiyo alitangaza kuwa Maria angehusika tena kwenye shoo ya sultana ambayo wengi wamekuwa wakisubiri.

Maria sasa yuko kwenye televisheni tena, jambo ambalo limewaacha wengi wakizungumza na kufurahia sana.

Amekuwa kimya tangu iliporipotiwa kuwa aliposhirikishwa katika kipindi cha sultana.

Kupitia kwenye ukurasa wake rasmi wa Instagram, akizungumzia hilo alisema kuwa anafurahi sana hatimaye kukutana tena namashabiki wake na sasa wanaweza kumtazama kwenye sultana kila Jumatatu hadi Ijumaa saa moja unusu usiiku.

"Nina furaha sana hatimaye kushiriki na nyinyi kwamba unaweza kumtazama MARIA kwenye SULTANA 😁," Aliandika Maria.