Mwimbaji wa Bongo Rajab Abdul Kahali almaarufu Harmonize amejawa na furaha baada ya makamu rais wa Marekani, Kamala Harris kuorodhesha wimbo wake 'Single Again' miongoni mwa nyimbo zake pendwa za wasanii wa Afrika.
Siku ya Jumatatu, Kamala Harris alitoa orodha rasmi ya miziki yake pendwa ya Afrika kwenye mtandao wa Spotify kama njia ya kupigia debe safari yake ya sasa katika bara, kulingana na jarida la Billboard.
"Orodha ya muziki, yenye jina la "Safari Zangu: Ghana, Tanzania, na Zambia," inapatikana kwenye jukwaa la utiririshaji, na imeundwa ili "kukuza wasanii na sauti kutokana na safari zangu" katika nchi hizo," alieleza.
Wimbo wa Konde Boy 'Single Again' ulikalia nafasi ya nane kwenye orodha ya nyimbo pendwa za makamu rais huyo wa Marekani.
Huku akijibu, bosi huyo wa Kondegang alimshukuru Harris kwa kutambua vipaji maalum kutoka bara la Afrika.
"Inafurahisha sana kwa Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris kutambua vipaji vya Afrika," alisema kwenye Instagram.
Mwimbaji huyo wa Muziki Bongo aliendelea kudhihirisha kuhusu uhusiano mzuri uliopo kati ya Marekani na Tanzania huku akimkaribisha msaidizi huyo wa rais Joe Biden katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.
"Uhusiano kati ya Tanzania & Marekani ni moja ya fahari yetu. Tafadhali jisikie uko nyumbani unapokuja kutembelea. Ni heshima sana," alisema.
Makamu wa rais wa Marekani aliwasili Ghana siku ya Jumapili, Machi 26, kwa safari yake ya kwanza barani Afrika akiwa ofisini, na atazuru Tanzania Jumatano na Zambia siku ya Ijumaa kabla ya kurejea Marekani Jumapili.
VP Harris aliratibu orodha ya kucheza kwa kushirikisha wasanii wa Ghana na wengine wenye asili ya Marekani kama Amaarae, Moses Sumney na Black Sherif; Wasanii wa Tanzania walio kwenye orodha ni pamoja na Harmonize, Zuchu na Alikiba; Kutoka Zambia kuna Chile One Mr. Zambia, Yo Maps na Chef 187.
Hii hapa ni orodha rasmi ya wasanii na ngoma zao pendwa alizozitaja naibu rais Harris.
- All My Cousins, “Act a Fool”
- Moses Sumney, “Me in 20 Years”
- T’neeya, “Pretty Mind”
- Amaarae, “Reckless & Sweet”
- Herman Suede, “Kumbaya”
- Moliy, “Ghana Bop”
- Ria Boss, “Call Up”
- Harmonize, “Single Again”
- Chile One Mr Zambia, “I Love You”
- Black Sherif, “Kwaku the Traveller”
- Jux, Marioo, Papi Cooper & Tony Duardo, “Nice (Kiss)
- Zuchu, “Utaniua”
- Yo Maps, “Aweah”
- Alikiba, “Mahaba”
- Jay Melody, “Sawa”
- Mbosso feat. Costa Titch & Alfa Kat, “Shetani”
- Sarkodie feat. Black Sherif, “Country Side”
- Platform Tz & Marioo, “Fall”
- Darassa feat. Bien, “No Body”
- Chef 187 & Blake, “Nobody”
- Kuami Eugene & Rotimi, “Cryptocurrency”
- Coolguy Pro, “Cherry”
- Marioo & Abbah, “Lonely”
- M3NSA, “Fanti Love Song”
- Baaba J, “Lumumba”