'Ogopa wanawake,'Crazy Kennar asema katika ujumbe wa kimafumbo

Crazy Kennar amewaacha mashabiki wake katika hali ya kuchanganyikiwa

Muhtasari
  • Wakenya wameibua wasiwasi kuhusu kile kinachoweza kuwa kinaendelea kwa Crazy Kennar kufuatia ujumbe wake wa kimafumbo ambao umeenea mitandaoni

Crazy Kennar ni mtayarishaji maudhui maarufu nchini Kenya. Amekuwa akitumia mtandao kuonyesha mbwembwe na maudhui yake ya kibunifu ambayo yamekuwa yakivuma kila mara na kuzua kicheko miongoni mwa Wakenya na hivyo kuondoa huzuni.

Crazy Kennar siku zote amekuwa moja kwa moja katika kueleza hisia zake na heka heka zake akiwa katika tasnia ya burudani.

Katika tukio la hivi punde, Wakenya wameibua wasiwasi kuhusu kile kinachoweza kuwa kinaendelea katika maisha ya Crazy Kennar kufuatia ujumbe wake wa kimafumbo ambao alichapisha mitandaoni.

Katika chapisho la hivi punde zaidi, Crazy Kennar amewaacha mashabiki wake katika hali ya kuchanganyikiwa huku wakishindwa kile ambacho wanawake wamemfanyia kufuatia chapisho lake akitahadharisha watu kuhusu wanawake.

Kupitia kwenye ukurasa wake rasmi wa Instagram aliandika;

"Ogopa wanawake Wooiii hata hangengoja january ifike tarehe 15 😂😂😂😂😂😂,"Kennar Aliandika.