logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Ondoka dakika 2 tu" Samidoh atoa ombi la unyenyekevu kwa Diamond

Siku mbili zilizopita alitoa wimbo wake mpya zaidi "bado nakupenda" akimshirikisha prince Indah

image
na Radio Jambo

Yanayojiri13 February 2023 - 10:48

Muhtasari


  • Ni kibao kinachozungumzia mwanamume aliyekuwa na hisia kwa mwanamke ilhali mwanamke huyo hamtaki wala kumpenda
Samidoh atoa ushauri kuhusu wanaume wa vitenge

Msanii wa mugithi Samuel Muchoki almaarufu Samidoh kupitia kwenye ukurasa wake facebook amemwambia Diamond Platnumz anapaswa kumwondokea dakika 2 tu kwenye youtube baada ya kibao chake kuvuma katika nambari 2.

Siku mbili zilizopita alitoa wimbo wake mpya zaidi "bado nakupenda" akimshirikisha Prince Indah ambaye ni mwanamuziki maarufu wa Ohangla.

Ni kibao kinachozungumzia mwanamume aliyekuwa na hisia kwa mwanamke ilhali mwanamke huyo hamtaki wala kumpenda.

Wimbo huo uliwaacha wengi wakiwa na furaha ambao ulifanya kuwa wa pili kuvuma kwenye YouTube, nyuma ya wimbo mpya wa Diamond ‘Zuwena’.

Dakika chache zilizopita Samidoh aliweka screenshot ya wimbo wote wa Diamond na wimbo wake akimwambia aondoke Diamond ili kuwatengenezea njia ndugu zake wawe wa kwanza kutrend kwa dakika mbili tu kisha atarudi.

Aliendelea na kuwashukuru wafuasi wake na kumuomba Mungu awabariki kwa msaada wao mkubwa katika maudhui yake.

"@mainawakageni tafadhali ambia rafiki yako @diamondplatnumz aondokee ndugu zake wadogo tuingie hiyo nafasi dakika mbili tu 👌halafu atarejea😜😂😂😂Kwa mashabiki maulana awazidishie baraka zake!🙏🙏."


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved