"Sina nguvu ya kucheat!" Muigizaji Abel Mutua afichua siri iliyodumisha ndoa yake ya miaka 14

Mutua alikuwa na miaka 22 na mkewe alikuwa 21 walipojitosa kwenye mahusiano.

Muhtasari

•Mutua amefichua kuwa urafiki mkubwa uliopo kati yake na mkewe ndio umeshikilia mahusiano yao ya miaka kumi na minne.

•Mutua alisema kwamba nyumbani kwake ndiko mahali pekee ambapo huwa anapata amani anayohitaji maishani.

katika hafla ya awali.
Muigizaji Abel Mutua na mke wake Judy Nyawira katika hafla ya awali.
Image: INSTAGRAM// JUDY NYAWIRA

Muigizaji mashuhuri Abel Mutua ameweka wazi kuwa Bi Judy Nyawira sio mke wake tu bali pia ni rafiki wake mkubwa.

Mutua amefichua kuwa urafiki mkubwa uliopo kati yake na mkewe ndio umeshikilia mahusiano yao ya miaka kumi na minne.

Wawili hao walikutana mwaka wa 2008 wakiwa bado vijana wadogo na wamekuwa pamoja tangu wakati huo.kutamania.

"Hii kitu huwa rahisi sana. Ingia kwa mahusiano na mtu ambaye wewe ni beshte yake. Kama hakuna urafiki, hiyo kitu ya mapenzi mnadanganyana mko nayo itaisha baada ya miaka mbili. Lakini mkiwa marafiki, ata hiyo kutamaniana ikiisha, urafiki wenu ndio huwaweka pamoja. Hiyo ndiyo kitu imetuweka pamoja. Mimi ata nikiwa na siku mbaya, siwezi kusubiri kufika nyumbani ndio niende nimwambie jinsi kumekuwa," Mutua alisema katika mahojiano na Eve Mungai.

Muigizaji huyo wa zamani wa Tahidi High alikuwa na umri wa miaka 22 na mkewe alikuwa na miaka 21 walipojitosa kwenye mahusiano.

Ameleza kuwa yeye na Bi Nyawira wamewahi kupitia mengi pamoja na kamwe hatamani kuanza upya na mtu mwingine.

"Kuanza hii kitu tukiwa wadogo tumepitia mengi mpaka huwa nawaza yaani nitaacha huyo mtu niende nianze mapambano na mtu mwingine? Hapana, acha ikae," Alisema.

Mutua alisema kwamba nyumbani kwake ndiko mahali pekee ambapo huwa anapata amani anayohitaji maishani.

Aliweka wazi kwamba kamwe hawezi kutoka nje ya ndoa yake kwani kwake hiyo ni kazi ngumu ambayo  inachokesha.

"Haiwezi, mimi najua sina hiyo nguvu ya kuanza kucheat," Mutua alisema.

Katika miaka ya mwanzo ya mahusiano yao, Bi Nyawira alipata ujauzito na kujifungua mtoto wa kike ambaye walikubalana kulea pamoja.

Mutua alisema alifurahia sana kumuona bintiye kwa mara ya kwanza kwani aliona akifanana na marehemu mama yake.