Willy Paul apanda bei, afichua ada zake mpya za juu

Ili kutumbuiza katika klabu iliyo jijini Nairobi, sasa anatoza ada ya Ksh 600,000.

Muhtasari

•Mapromota watakaomtaka aonekane tu kwenye klabu bila kutumbuiza watalazimika kulipa Sh300,000.

•Wamiliki wa makampuni watalazimika kumlipa shilingi milioni 30  ili kuwa balozi wa bidhaa zao.

Image: INSTAGRAM// WILLY PAUL

Mwimbaji Wilson Radido almaarufu Willy Paul ameobgeza  ada ya huduma zake.

Siku ya Jumamosi, mwimbaji huyo wa nyimbo za injili wa zamani alifichua kadi yake mpya ya kazi  iliyo na ada mpya za aina tofauti za huduma anazotoa.

"Kadi yangu ya bei iliyosasishwa" aliandika kwenye Instagram.

Kulingana na kadi hiyo mpya, mapromota watakaomtaka aonekane tu kwenye klabu bila kutumbuiza watalazimika kulipa Sh300,000.

Ili kutumbuiza katika klabu iliyo jijini Nairobi, Willy Paul  sasa anatoza ada ya Ksh 600,000.

Itagharimu Ksh 200,000 kuweka tangazo moja kwenye Instastori za mwimbaji huyo. Kufanya matangazo kwenye ukurasa wake wa Instagram  itagharimu shilingi nusu millioni kwa kila chapisho.

Wamiliki wa makampuni watalazimika kumlipa shilingi milioni 30  ili kuwa balozi wa bidhaa zao.

Willy Paul pia anatoza Ksh shilingi milioni moja unusu ili kutumbuiza katika hafla yoyote ya nje. Wanaohitaji huduma zake wameagizwa kuwasiliana naye kupitia saldido@gmail.com.

Image: INSTAGRAM// WILLY PAUL

Haya yanajiri siku chache tu baada ya msanii huyo aliyezingirwa na utata mwingi kujigamba kuhusu umahiri wake unaomfanya awe na kiburi.

Willy Paul alisema  kuwa yeye hajali watu wanasema nini kwani hakuna anayempatia chakula wala kitu chochote.

 "Si hakuna mtu ananilisha? Alafu si niko na pesa na maisha fiti alafu mimi ni  Mluo mzuri! " Alijigamba Willy Paul.

Aliendelea kuwachana wasanii wenzake kwa kudai kuwa hakuna anayekaribia kiwango chake, hivyo sababu nyingine ya yeye kujivunia.

Zaidi ya hayo, mimi ndiye mwanamuziki mahiri zaidi hapa Kenya.... Baaass!" alisema Pozze.

Wiki chache zilizopita mwimbaji huyo alionyesha magari yake katika kile kilichoonekana kama jibu kwa wakosoaji wake. Hapo awali alizindua Mercedes Benz mpya ya rangi ya majano.