Mbunge Peter Salasya akutana na mwanadada aliyemuomba amuoe, amuuliza kama ni bikira

Mwanadada huyo alisisitiza yuko tayari kwa ndoa na kwamba yuko tayari kukaa kijijini wakati mumewe anafanya kazi Nairobi

Muhtasari

•Mbunge Peter  Salasya mnamo Jumanne hatimaye alikutana na mwanadada kutoka Kakamega ambaye alibeba bango akimuomba amuoe.

•Salasya alipomuuliza mwanamke huyo ni nini kilimvutia zaidi kwake, alisema “Nadhani tunaendana.Tunarhyme. Baada ya muda utajua.”

alikutana na mwanadada aliyemuomba amuoe.
Mbunge Peter Salasya alikutana na mwanadada aliyemuomba amuoe.
Image: INSTAGRAM// PETER SALASYA

Mbunge wa eneo la Mumias Mashariki Peter Kalerwa Salasya mnamo Jumanne hatimaye alikutana na mwanadada kutoka Kakamega ambaye alibeba bango akimuomba amuoe.

Hivi majuzi, Bi Lavyn Shantell alionekana barabarani akiwa amebeba bango lililoandikwa ‘Mbunge PK Salasya marry me. Niko tayari kusettle’ na hata akaandika maelezo yake ya mawasiliano.

Kwa kweli, juhudi za mwanadada huyo zilimfanya akutane na mbunge huyo wa muhula wa kwanza kwenye mkahawa mmoja wa chakula mjini Kakamega mnamo Jumanne.

“Habari zenu, hatimaye nimekutana na mume wangu. Nina furaha sana. Nahisi kama nimefarijika, kana kwamba niko sawa. Tuko hapa tunakula chakula cha jioni,” Bi Lavyn alisema kwenye video ya mkutano wao iliyochapishwa a na mbunge huyo kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Lavyn alifichua kuwa mwanasiasa huyo alimnunulia mlo wa ugali na kuku.

Mbunge Salasya alipomuuliza mwanamke huyo ni nini kilimvutia zaidi kwake, alisema “Nadhani tunaendana.Tunarhyme. Baada ya muda utajua.”

Mwanamke huyo alisisitiza kuwa yuko tayari kwa ndoa na akabainisha kuwa yuko tayari kukaa kijijini wakati mumewe anafanya kazi Nairobi.

“Basi waambie wanachama wa mitandaoni kwamba umetosha. Alafu tuone, mtandao ikikubali tutaona mambo yako. Mtandao ukikataa basi ndo hivyo,” Salasya alimwambia Lavyn.

Swali lingine ambalo mbunge huyo alimuuliza mrembo huyo ni iwapo bado ni bikira.

Bi Lavyn akajibu, "Utajua baadaye."

Hapo awali, mwanasiasa huyo mcheshi alikuwa amekataa ombi la ndoa kutoka kwa mwanamke huyo ambaye alijitolea kuwa mke wake.

Kulingana na Salasya, alisema kuwa hawezi kumshughulikia kutokana na mwonekano wake wa kimwili.

"Nimesikia kwamba hii inavuma na sina uhakika kama ninaweza kushughulikia hii machine," Salasya aliandika kwenye chapisho lake la facebook.