"Mwijaku alilia usiku kucha aende!" Sababu ya H-Baba kuachwa na Diamond akienda Qatar yafichuliwa

Mwimbaji huyo alidai kuwa Mwijaku ndiye alisababisha yeye kuachwa nyuma.

Muhtasari

•Diamond alisafiri siku ya Jumatatu na aliandamana na kundi la wanafamilia,  marafiki na baadhi ya washirika wake.

•H-Baba alifichua kwamba yeye ni miongoni mwa watakaosafiri katika awamu ya pili.

H-Baba akimsalimia bosi wake Diamond.
Image: INSTAGRAM// H-BABA

Mwimbaji wa Bongo na ambaye ni balozi wa Wasafi Bets H-Baba ametetea kuachwa nyuma kwake wakati bosi wake Diamond Platnumz akisafiri kuelekea Qatar ili kushuhudia moja kwa moja mechi za Kombe la Dunia.

Diamond alisafiri kwa ndege kutoka Tanzania hadi nchi hiyo ndogo ya Asia siku ya Jumatatu na aliandamana na kundi la wanafamilia,  marafiki na baadhi ya washirika wake. H-Baba hata hivyo hakuwepo ndani ya ndege hiyo.

Katika mahojiano na Bongo Touch, msanii huyo wa zamani wa Harmonize alibainisha kuwa aliachwa nyuma kwa kuwa wote ambao wameratibiwa kuenda Qatar kwa ufadhili wa kampuni hiyo hawangeweza kusafirishwa wote katika awamu ya kwanza.

"Wamesema kuna awamu ya pili. Tukisafiri wote katika awamu ya kwanza wasafiri nani katika awamu ya pili," alisema.

H-Baba ambaye alianza kufanya kazi na Diamond mapema mwaka huu alifichua kwamba yeye ni miongoni mwa watakaosafiri katika awamu ya pili.

Hata hivyo, alikiri kuwa alitaka kusafiri katika awamu ya kwanza huku akidai kwamba Mwijaku ndiye alisababisha yeye kuachwa nyuma.

"Kwenye awamu ya kwanza nilitaka niende mimi na Baba Levo. Mwijaku alikuwa analia usiku kucha kwa sababu hajawahi kusafiri kuenda nje. Alikuwa anampigia Ricardo Momo usiku, hajalala kaka huyo wa Diamond," alisema.

Alisema kuwa alikubali kuacha nafasi yake kwa mchekeshaji huyo  na akaomba aende katika awamu ya pili.

"Mimi na Madonga tutaondoka pamoja katika awamu ya pili. Nilijiskia vibaya kusikia kuwa ndugu yangu Mwijaku hajawahi kusafiri ata siku moja. Ni safari yake ya kwanza. Pasipoti yake haina ata muhuri mmoja," alisema.

H-Baba alimshtumu balozi huyo mwenzake kwa kuwa na unafiki mwingi katika utendakazi wake.

Miongoni mwa walioandamana na bosi huyo wa WCB katika safari hiyo ni pamoja na Mama Dangote na mpenzi wake Uncle Shamte, Esma Platnumz, Mbosso, meneja Ricardo Momo, msemaji wa Yanga S.C Haji Manara, Baba Levo, Mwijaku pamoja na mlinzi rasmi wa Diamond Onesmo Amos.

Pamoja nao katika ndege hiyo walikuwepo Watanzania wengine sita waliofadhiliwa na Wasafi Bet yake Diamond. W

Wote hao walirejea Tanzania siku ya Alhamisi.