logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Ni wewe pekee" Rayvanny amhakikishia mkewe Fahyma baada ya kukabiliana na Paula mtandaoni

Rayvanny na Fahyma walirudiana mwezi uliopita baada ya kutengana kwa takriban miaka mitatu.

image
na Radio Jambo

Habari23 May 2023 - 08:04

Muhtasari


•Rayvanny ametumia jukwaa lile lile ambalo alitumia kumtukana Paula kumhakikishia Paula kuwa yeye ndiye mwanamke pekee katika maisha yake.

•Wakati wa mzozo wao, Rayvanny na Paula walinyoosheana vidole kuhusu mahusiano yao yaliyovunjika mwaka jana.

Baada ya kutupiana cheche za maneno na mpenzi wake wa zamani Paula Kajala, staa wa bongo Raymond Shaban Mwakyusa almaarufu Rayvanny amemhakikishia mke wake Fahymah kuhusu upendi wake mwingi kwake.

Siku ya Jumatatu jioni, bosi huyo wa lebo ya Next Level Music ametumia jukwaa lile lile ambalo alitumia kumtukana Paula kumhakikishia mzazi mwenzake kuwa yeye ndiye mwanamke pekee katika maisha yake.

"Ni wewe pekee," Rayvanny aliandika chini ya picha yake na Fahyma ambayo alichapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Aliambatanisha ujumbe huo na emoji za moyo wenye moto kuashiria mahaba mazito aliyo nayo kwa mkewe.

Katika jibu lake, mama huyo wa mvulana mmoja alimthibitishia Rayvanny kwamba anampenda sana pia.

"Nakupenda, nakupenda tena #MaishaYangu," alijibu.

Jioni hiyo hiyo, Rayvanny na Paula walipigana vita vya maneno kwenye mtandao huo ambapo waliibua madai mazito dhidi ya kila mmoja.

Wakati wa mzozo wao, wasanii hao wawili wa bongo walinyoosheana vidole kuhusu mahusiano yao yaliyovunjika mwaka jana.

Rayvanny ambaye alirudiana na  Fahyma hivi majuzi alidai kwamba binti huyo wa Kajala Masanja alimsaliti kimapenzi na nduguye.

"Nilijua unalala na kakangu niliyemheshimu sana kwenye mziki wangu na unajua tunaheshimiana sana, hapo ndipo nilibadilisha mawazo," Rayvanny alisema.

Paula hata hivyo alibainisha kwamba hakuwahi kumsaliti bosi huyo wa Next Level Music wakati wa mahusiano yao ya mwaka mmoja.

Aidha, alidai kuwa mwenzake Rayvanny hata hivyo hakuwa mwaminifu kwani angem'cheat na mzazi mwenzake, Fahyma.

"Nilikaa na wewe mwaka mzima kila mtu anajua tumeachana wakati ulikuwa na mimi na mwanamke wako. Ulitaka niendelee kukaa na wewe wakati unanificha  ficha ukienda kwa mwanamke wako unasema nakusumbua, ukija kwangu unasema mwanamke wako anakusumbua," Paula alijibu.

Mwanamitindo huyo wa miaka 20 alimbainishia Rayvanny kuwa alifahamu matendo yake na ndiposa akachukua hatua ya kumuacha.

"Acha kufanya watu waonekane mbaya. Unajua nilijitolea vingapi kwaajili ya haya mahusiano?? Mbona husemi marafiki zangu ulivyolala nao kwenye gari lako," Paula alimuuliza mpenzi huyo wake wa zamani.

Paula alimtaka mwanamuziki huyo kukoma kumchafulia jina kwa madai mazito dhidi yake na kumwagiza atoe ushahidi wowote kuthibitisha kwamba alimsaliti kimapenzi na ndugu huyo wake asiyefichuliwa. Alidai kwamba Rayvanny aliwahi kumsaliti na baadhi ya marafiki zake pamoja na wapenzi wa marafiki wake.

Rayvanny kwa upande wake alisisitiza alimtafuta binti huyo wa Kajala kwa ajili ya mapenzi na kumpongeza kwa mahusiano yake ya sasa.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved