Mwaka wa 2023 unakaribia kuisha, ni siku chache tu zimesalia ili tuweze kuukaribisha mwaka mpya wa 2024.
Huku mwaka ukilekea ukingoni, sio mwaka pekee unaoisha, pia umekuwa mwisho wa ndoa na mahusiano mengi.
Mojawapo ya misambaratiko mikuu iliyoshangaza taifa ni ile ya mwimbaji Akothee na mumewe Denis ‘Omosh’ Schweizer ambao ndoa yao iligonga mwamba miezi miwili tu baada ya kufanya harusi. Wawili hao walikuwa wakichumbiana kwa muda kabla ya kufanya harusi mnamo Aprili kisha wakaachana mwezi Juni.
Mwanasholaiti Vera Sidika na mzazi mwenzake Brown Mauzo ni wanandoa wengine walioshangaza taifa kwa kutengana baada ya miaka miwili ya uchumba. Wawili hao waliachana miezi michache tu baada ya kuzaliwa kwa mtoto wao wa pili, Ice Brown.
Hii hapa orodha ya mastaa mbalimbali wa Kenya walioachana mwaka wa 2023;
- Akothee & Denis ‘Omosh’ Schweizer
- Vera Sidika & Brown Mauzo
- Tyler Mbaya na Georgina Njenga
- Jackie Matubia na Blessing Lung’aho
- Kate Actress & Phillip Karanja
- Lupita Nyong'o na Selema Masekela
- Weezdom na Mylee Stacey
- Ajib Gathoni na Josh Wonder
- Amber Ray & Kennedy Rapudo (Walirudiana)