logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Orodha ya zawadi za thamani ambazo Diamond Platnumz alimpa mtangazaji wake katika harusi yake

Diamond aliahidi kumwongeza mtangazaji huyo mshahara kwa asilimia hamsini.

image
na Radio Jambo

Makala26 March 2022 - 09:37

Muhtasari


•Diamond alipopewa nafasi ya kutoa hotuba yake alichukua fursa hiyo kumpongeza mfanyikazi huyo wake kwa kazi kubwa ambayo amekuwa akifanya Wasafi.

•Diamond aliagiza msaidizi wake Don Fumbwe kupatia wanandoa hao kipande chake cha ardhi kilicho karibu na bahari katika eneo la Kigamboni.

Diamond Platnumz na Diva the Bawse

Mnamo Ijumaa, staa wa Bongo Diamond Platnumz alihudhuria harusi ya mtangazaji wa Wasafi Media, Diva The Bawse.

Diva ambaye ni mtangazaji wa kipindi cha Lavi Davi alifunga pingu za maisha na mumewe Sheikh Abdulrazak Salum katika hoteli ya Hyatt Regency Hotel, Dar es Salaam.

Diva na mumewe Abdul

Diamond alipopewa nafasi ya kutoa hotuba yake alichukua fursa hiyo kumpongeza mfanyikazi huyo wake kwa kazi kubwa ambayo amekuwa akifanya Wasafi.

"Kiukweli, toka ulipokuja Wasafi Media, haujawahi kutuangusha. Shughuli unayoifanya pale, ni kipindi uko peke yako lakini unaifanya ikae ni kama mko watu ishirini.Unaifanya bora, kila mtu lazima akisikilize. Sio kazi rahisi, ni kazi kubwa, inahitaji mtangazaji ambaye ana akili, ana talanta ya kweli lakini pia anatumia muda kukaa nyumbani na kufikiria vitu anavyovifanya," Diamond alisema.

Kutokana na kazi yake  nzuri, Diamond aliahidi kumwongeza mtangazaji huyo mshahara kwa asilimia hamsini.

Bosi huyo wa WCB pia aliahidi kumpatia Diva the Bawse runinga mpya, simu mbili mpya  na ugavi wa kila mwezi wa soda.

Isitoshe, Diamond aliagiza msaidizi wake Don Fumbwe kupatia wanandoa hao kipande chake cha ardhi kilicho karibu na bahari katika eneo la Kigamboni.

"Na millioni kumi kesho uwawekee kwenye akaunti," Diamond alisema.

Diva alianza kufanya kazi katika Wasafi Media mwaka wa 2020 baada ya kujiuzulu kutoka Clouds Media ambako alihudumu kwa zaidi ya mwongo mmoja.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved