"Pumzika kwa amani Shem!" Mpenzi wa Eric Omondi ajawa huzuni kufuatia kifo cha shemeji yake, Fred Omondi

Aliambatanisha ujumbe wake na emojis ambazo hutumiwa kuonyesha huzuni.

Muhtasari

•Mpenzi wa mchekeshaji Eric Omondi alionyesha masikitiko yake wakati  akiomboleza kifo cha shemeji yake Fred Omondi.

•“Pumzika kwa amani Shem,” Lynne aliandika chini.

Lynne, Fred Omondi na Eric Omondi
Kumbukumbu ya Lynne, Fred Omondi na Eric Omondi
Image: INSTAGRAM// LYNNE NJIHIA

Lynne Njihia, mpenzi wa mchekeshaji Eric Omondi alionyesha masikitiko yake wakati  akiomboleza kifo cha shemeji yake Fred Omondi.

Fred aliaga dunia siku ya Jumamosi asubuhi katika kile kilichoripotiwa kuwa ajali mbaya ya barabarani iliyotokea kwenye barabara ya Outering jijini Nairobi.

Huku akimuomboleza shemeji yake, Lynne alichapisha picha na video za kumbukumbu nzuri aliyokuwa nayo na marehemu katika siku za nyuma.

“Pumzika kwa amani Shem,” Lynne aliandika chini.

Aliambatanisha ujumbe wake na emojis ambazo hutumiwa kuonyesha huzuni, kuonyesha hali yake ya sasa kufuatia tukio hilo la kuhuzunisha. 

Katika video ambayo Lynne alishiriki, marehemu Fred Omondi alionekana akicheza densi kwa furaha huku muziki ukicheza kwa mbalii. Mpenziwe Lynne, Eric Omondi na watu wengine wasiojulikana pia walikuwepo katika tukio hilo lililoonekana kuwa maalum.

Kwa upande wake, mchekeshaji Eric Omondi alionyesha kuvunjwa moyo sana na kifo cha ghafla cha mdogo wake.

Huku akimuomboleza kaka yake kwenye Instagram, Eric alichapisha video ya wimbo wa kejeli ya kisiasa ambao walifanya pamoja wakati fulani nyuma.

Kisha akamuombea kaka yake apumzike kwa amani.

“Nenda vizuri kaka @fredomondi_,” Eric aliandika chini ya video hiyo na kuiambatanisha na emoji ya moyo uliovunjika, kuashiria hisia zake kwa sasa.

Eric na Fred walikuwa ndugu wa karibu sana na wote wawili walifanikiwasana katika tasnia ya burudani ya vichekesho.

Polisi walisema ajali iliyomuua Fred ilitokea Jumamosi asubuhi baada ya bodaboda iliyokuwa imembeba kugongwa na basi lililokuwa likienda mwendo kasi na kumlazimisha mwendeshaji huyo na marehemu kutua kwenye lami.

Omondi alikimbizwa katika Hospitali ya Mama Lucy ambapo alitangazwa kuwa amefariki alipokuwa akihudumiwa, afisa wa polisi alisema.

Shahidi alisema alifariki papo hapo.

Marafiki na watu mashuhuri waliotumbuiza naye walikusanyika kwenye mitandao ya kijamii kuomboleza kifo chake.

Mchekeshaji Terrence Creative alipokuwa akimuomboleza alisema alipokea simu saa kumi na mbili asubuhi Jumamosi kumjulisha kifo chake.

"Fred namshukuru Mungu kwa muda aliotupa pamoja bro, umekuwa sehemu ya kazi yangu na ukuaji katika tasnia. Ulinichukulia kama kaka na kunikaribisha wakati sikuwa na mahali pa kwenda," Terrence alisema.

"Ulinipa jukwaa na kunilipa, na kwa pamoja tulianza maonyesho ya vichekesho vya klabu. Nitathamini kila wakati tuliposhiriki jukwaa."

Mwanasiasa Millicent Omanga, alitoa rambirambi zake kwa X, akisema:

"Tasnia ya ubunifu imepoteza thamani. Fred Omondi aliangaza vyumba vyetu vya kuishi na vichekesho vyake vya uraibu. Kwamba amepoteza maisha yake katika ajali ya barabarani inahuzunisha moyo. Ninawapa pole familia yake, marafiki, na mashabiki wake. Naomb nafsi yake ipate amani kamili."

Mwanamuziki Nameless naye alimlilia.

“Hii imezidi... maisha ni tete! Pumzika vizuri Fred! Habari za kusikitisha kama hizo! Pole za dhati kwa familia!!