Mtayarishaji maudhui Ruth K ni mwanamke mwenye furaha tele baada ya mzazi mwenzake David Oyando almaarufu Mulamwah kupata gari lake la kwanza siku ya Alhamisi.
Mulamwah alifichua habari za fanikio hilo lake kubwa siku ya Alhamisi wakati ambapo alishiriki picha za gari zuri aina ya Mercedes Benz E250 alilonunua.
Wakati akitoa tangazo hilo, mchekeshaji huyo mwenye umri wa miaka 30 alimshukuru Mungu, familia yake na mashabiki kwa jukumu muhimu walilocheza katika mafanikio hayo.
“MUNGU ALIFANYA 💪🙏 mmiliki gari mwenye fahari 💯 mercedes BENZ E250 innit . kila mara tembea polepole lakini, sogea ipasavyo 💯. namshukuru Mungu kwa baraka zote maishani, wacha tuanzie ka life apa . shukrani kwa familia, mashabiki na marafiki kwa usaidizi wenu na maombi kila mara,” Mulamwah alisema.
Baba wa watoto wawili alidokeza kuwa gari hilo sasa litamsaidia mzazi mwenzake Ruth na mtoto wao mdogo kusafiri hadi kliniki kwa urahisi kila inapohitajika.
Pia hakusahau kumshukuru mpenzi wake kwa sapoti ambayo ameendelea kumpa.
“Kijana cha kitale sasa ni former pedestrian. kalamwah na mama kalamaz clinic wanafika in style sasa . @atruthk asante kwa support daima mamake,” alisema.
Ruth kwa upande wake alimsherehekea mpenzi huyo wake kwa kununua gari hilo maridadi na kumpongeza kwa mafanikio hayo.
"Hongera baba Kalamwah," Ruth K aliandika chini ya video yake akiwa amesimama kando ya gari nyeusi aina ya Mercedes.
Alibainisha kuwa Mulamwah anastahili sana gari hilo akifichua kwamba ilimchukua bidii, maombi na kujitolea kulinunua.
"Matokeo ya uvumilivu, maombi, bidii na kujitolea🎉🎉 hongera baba kalamz @oyando_jnr kwa ushindi huu♥️," aliandika.
Aliongeza, "Hii ni ya thamani ya kusubiri , Nisaidieni kumpongeza mmiliki mpya wa gari mjini🎉♥️anastahili sana. Ninafurahi na kujivunia wewe sana, nakupenda♥️.Road test unanipelek#a wapi🙈😋”
Mama huyo wa mvulana mmoja pia hakuweza kuficha jinsi anavyojivunia mpenzi wake.