Zari amfuta Diamond maishani mwake, amshutumu kwa kuharibu ndoa yake na kumtumia kupata wanawake

Mwanasosholaiti huyo alifichua kuwa madai ya Diamond dhidi yake yalisababisha mgogoro katika ndoa yake mpya na Shakib.

Muhtasari

•Zari alikanusha madai kuwa bado anampenda mwimbaji huyo wa Bongo na kwamba aliomba kuzaa naye mtoto mwingine.

•Mwanasosholaiti huyo alidai kuwa Diamond ndiye amepata ugumu wa kusonga mbele baada ya. mahusiano yao kuvunjika.

•Zari aliweka wazi kuwa uhusiano wao hautakuwa sawa tena na kubainisha kuwa anaweza kujisimamia  mwenyewe

amemfuta Diamond kutoka maisha yake.
Zari amemfuta Diamond kutoka maisha yake.
Image: INSTAGRAM

Mwanasosholaiti wa Uganda, Zari Hassan ni mwanamke mwenye hasira tele baada ya aliyekuwa mpenzi wake na mzazi mwenzake Diamond Platnumz kuibua madai kwamba bado anampenda na hata alitaka kupata mtoto mwingine naye.

Katika tukio moja kwenye filamu ya uhalisia iliyoachiwa siku ya Ijumaa, Young, Famous and African sehemu ya pili, Diamond Platnumz alisikika akimwambia mshikaji wake mpya, Francine Koffie almaarufu Fantana kutoka Ghana kwamba mpenzi wake wa zamani Zari Hassan alitaka mtoto wa tatu naye.

Staa huyo wa Bongo alidai kuwa Zari alitaka kupata mwanamke mwingine wa kumbebea mtoto wao wa tatu.

"Zari alitaka mtoto mwingine nami. Alitaka kupata mtu wa kumzalia mtoto," Diamond alimwambia mwimbaji huyo wa Ghana.

Katika majibu yake yaliyojaa machungu siku ya Jumamosi, Zari Hassan alikanusha madai kuwa bado anampenda mwimbaji huyo wa Tanzania mwenye umri wa miaka 32 na kwamba aliomba kuzaa naye mtoto mwingine.

Mwanasosholaiti huyo alidai kuwa Diamond ndiye amepata ugumu wa kusonga mbele baada ya. mahusiano yao kuvunjika.

"Mpendwa Ex, Ninakuheshimu sana kama baba wa watoto wangu na hakuna kinachoweza kuingilia kati ya hilo. Ikiwa kungekuwa na nafasi ya sisi kurudi pamoja ungerudi mbio. Jinsi unavyokaa na wanawake (watu wa muda katika maisha yako) mkijadiliana mimi huniacha na mshangao. Unaweza kucheza na mtu yeyote unayemtaka bila kunitumia kama dau," Zari Hassan alilalamika katika taarifa.

Aliongeza, "Sikutaki, sijapagawa na wewe, kwa kweli ni kinyume chake. Umepagawa na mimi, inaonekana huwezi kupata wa kuchukua nafasi yangu. Utakuja mbio kama duma nikikuita urudi. Ninaelewa tu kwa sababu ya heshima kwa ajili ya watoto."

Mama huyo wa watoto watano alisema kuwa mwimbaji huyo wa Tanzania atakuwa katika maisha yake daima kwa sababu ya watoto wao. Hata hivyo aliweka wazi kuwa mambo hayatakuwa kawaida tena kufuatia tukio hilo la Netflix.

"UMESIMAMISHWA, na ikiwa hupendi, acha mahakama iamue. Sikuhitaji, pamoja na au bila wewe, nina MAISHA MZIMA. Mara ya mwisho niliangalia EA nzima hukujulikana hadi nilipokutambulisha kwenye tasnia. Nilikuwa milionea maarufu, nikiendesha magari ya Porsche, nikimiliki mali, smart na mrembo," alimwambia Diamond.

Mwanasosholaiti huyo mwenye umri wa miaka 42 alimshutumu Diamond kwa kuwaruhusu wapenzi wake wadogo kutomheshimu ili tu kulala nao.

Pia alifichua kuwa madai ya staa huyo wa Bongo dhidi yake yalisababisha mgogoro katika ndoa yake mpya na Shakib.

"Mimi ni mwanamke aliyeolewa hivi sasa na madai yako hayakukaa vizuri na ndoa yangu. Shoo kuhariri tu sehemu zinazowafaa ni upuuzi. NILIWEKA WAZI MIMI NIKO NA MTU SASA, siwezi kuzaa na wewe," Alisema.

Zari Hassan pia alimshtumu mpenzi huyo wake wa zamani kwa kupenda kutafuta kiki sana na kujinufaisha na drama.

Kutokana na hayo, aliweka wazi kuwa uhusiano wao hautakuwa sawa tena na kubainisha kuwa anaweza kujisimamia  mwenyewe.