Liverpool, Man City na Chelsea miongoni mwa timu zinazotaka huduma za Neymar

Liverpool, Manchester City na Chelsea ni miongoni mwa timu sita zinazotaka kumsaini mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil na Paris St-Germain Neymar, 27, na mchezaji mwenzake Kylian Mbappe, 20. (Le Parisien, via Mirror)

Mbappe ambaye ni mshambuliaji wa Ufaransa hana mpango wa kusaini kandarasi mpya PSG mkataba wake wa sasa ukimalizika mwisho wa mwaka 2022. (Marca)

Carlo Ancelotti ndiye chaguo la Everton atakayemrithi Marco Silva kama mkufunzi baada ya Mtaliano huyo kufutwa kazi na Napoli usiku wa Jumanne. (Telegraph)

Carlo Ancelotti alipigwa kalamu na Napoli usiku wa Jumanne

Manchester City inamhitaji beki mpya na tayari imejiunga na foleni ya usajili wa nyota wa Ufaransa Samuel Umtiti, 26, kutoka Barcelona. (L’Equipe, via TEAMtalk)

Wakimkosa Umtiti, Manchester City itaelekea Bournemouth kumtafuta Nathan Ake, 24, lakini huenda wakakabiliwa na ushindani kutoka kwa Chelsea. (Express)

Beki wa England Fikayo Tomori, 21, anakaribia kusaini mkataba mpya Chelsea. (Goal)

Zlatan Ibrahimovic huenda akarejea tena katika ligi ya Premia baada ya Everton kumpatia ajenti wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uswidi wa miaka 38-ofa ya £4m. (Express)

Manchester United huenda ikamkosa kiungo wa kati wa England James Maddison, 23, ambaye anakaribia kutia saini mkataba mpya ulioimarishwa Leicester City. (Mirror)

Roman Abramovich amepuuzilia mbali ofa kutoka kwa mmiliki wa LA Dodgers, odd Boehly kununua klabu ya Chelsea. (Telegraph)

Jame Maddison

Mkufunzi wa Inter Antonio Conte anataka Chelsea imuachilie beki wa nyuma na kushoto Mhispania Marcos Alonso, 28, ili aungane nae Italia huku winga Pedro, 32, na mshambuliaji wa Ufaransa Olivier Giroud, 33, pia wakitarajiwa kuondoka Stamford Bridge. (Goal.com)

Barcelona wamesitisha mpango wa kumnunua mshambuliaji wa Inter Milan na Argentina Lautaro Martinez, 22 kutokana na bei ya 100m euro (£84.6m. (ESPN)

-BBC

Picha za familia ya John, simu ya kukutana na babake aliyefariki Mombasa CBD

Marehemu John Mutinda aliishi maisha mazuri kwa mujibu wa picha za familia yake na jumba aliloishi.

John Mutinda in the office

Kisa cha John kiliteka vichwa vya habari baada tya kutumbukia bahari Hindi.

Taarifa zinasimuliwa kuwa ndoa yake ilikuwa na matatizo chungu nzima.

Niacheni ! Naomba utulivu niomboleze mume wangu, Ruth Mueni

Aidha, mkewe amenukuliwa kusema kuwa John alipigiwa simu na babake aliyefariki kitambo wakutane katikati mwa jiji la Mombasa.

John Mutinda and his kids

Mkewe Ruth Mueni na mamake wanaonekana kuchukua mitazamo tofauti kuhusu kifo cha John Mutinda.

The late John Mutinda and his family outside their home

Ruth anasingizia nguvu za giza katika kuelezea sababu za kifo cha mumewe ilhali mamake John anasema kuwa mumewe alikuwa ananyanyaswa kiakili katika ndoa hiyo.

(+Picha) Mchumba wa mcheshi Dr Ofweneke aonyesha ujauzito wake

“Mwanangu alifariki kutokana na kuzongwa na fikra iliyosababishwa na mkwamba alikuwa ameingiwa na kichaa,” alisema mama huyo wakati wa mahojiano naatatizo yaliyokuwa katika ndoa yake. Ni vibaya mkewe kusema alikuwa punguani…” Mamake John aliifungukia Taifa Leo.

Ila je ni nani anasema ukweli?

The late John Mutinda waters his plants

Hii inaashiria kuwa ndoa nyingi zimevurugika na mahusianio mema kuota mbawa.

Kisa kama hiki sio kizuri kwani kinaweza kikasababisha wanandoa kuuana.

The late John Mutinda and his family at the beach

 

Je, una mazoea ya kununua matunda na kuyala barabarani? Tazama hii video

Watu wengi sana hununua matunda yanayouzwa na wachuuzi barabarani na kuyala hususan wanapokuwa safarini.

Ijapokuwa matunda ni mojawapo ya viungo muhimu ya lishe bora, yanaweza yakasababisha maradhi hatari mwili.

Mwanaume Auawa Na Simba Huku KWS Ikitoa Tahadhari

Katika kanda ya video hii, mchuuzi anaonekana akiyaosha matunda kwenye maji chafu ya mtaro kando ya barabara.

 

Aidha, baada ya kuyaosha, lengo lake ni kwenda kuyauzia wapita njia au hata abiria walio na kiu ya kuyala matunda.

Hivyo basi, unafaa kuwa mwangalifu sana, usije ukajipatia maradhi hatari zaidi kutokana na maji taka yatumiwayo kuosha matunda hayo.

PATANISHO: Sipendi Tabia Za Mume Wangu Za Kuskiza Watu!

Niacheni ! Naomba utulivu niomboleze mume wangu, Ruth Mueni

Mkewe marehemu John Mutinda amezitaka vyombo vya habari kumpa amani na wakati mtulivu wa kuomboleza mwanawe.

Kisa cha John kujitosa na kufa maji Bahari hindi kilingonga vichwa vya habari huku wengi wakiwa na lengo la kujua sababu zilizochangia marehemu kujiua.

Ndoa ya marehemu na mkewe Ruth Mueni inasimuliwa kuwa na matatizo yanayokisiwa kuwa yalichochea kujitoa uhai.

Image result for john mutinda ferry

Katika mahojiano na vyombo vya habari mama huyu amesema kuwa ana imani kuwa mwanawe alijiua.

Aidha, mamake amisema kuwa mwanawe alikuwa anauguza majeraha ya kuchomwa kwa maji moto.

Mkewe John Mutinda aidha alizitaka vyombo vya habari kumkoma ili apate nafasi tulivu ya kumuomboleza mumewe.

Mwili wa mwendazake ulitolewa baharini saa mbili na dakika arobaini asubuhi siku hiyo hiyo.

Mamlaka ya huduma za feri nchini ilisema kuwa gari lake liliopolewa mwendo wa saa sita mchana.

Gari hilo lilipatikana mita 6 chini ya bahari Hindi.

Sio mara ya kwanza John kutaka kujiua, Carol Paul asema

Ndugu wa mwanamume aliyekufa maji Bahari Hindi amefunguka na kusema kuwa sio mara ya kwanza John kujaribu kujitoa uhai.

Carol Paul ameongeza na kusema kuwa sababu za John Mutinda kujitumbukiza katika bahari kulichochewa na kuzongwa na fikra kwa kipindi kirefu.

(+Picha) Mchumba wa mcheshi Dr Ofweneke aonyesha ujauzito wake

Ndoa ya marehemu na Ruth Mueni ilisheheni matatizo tele.

Image result for john mutinda ferry

Mutinda aliendesha gari lake kwa kasi baada ya kununua tiketi ya kuingia feri licha ya kusimamishwa na wathibiti wa kivuko hicho.

Mjane Ruth Mueni aliambia vyombo vya habari kuwa bwanake aliota kama amepigiwa simu na babake aliyefariki kitambo hivi kupelekea mauti yake.

Mimi ni bikra na sipo kwenye mahusiano na jinsia ya kike, Stivo Simple Boy

 

Ruth alisema kuwa bwanake na babake walikuwa wapatane katikati mwa jiji la Mombasa.
Image result for john mutinda ferry

Aidha, mamake John alikana taarifa hizo na kusema matatizo ya ndoa ndiyo yalichangia kijana wake kujiua.

Image result for john mutinda ferry

“Mwanangu alifariki kutokana na kuzongwa na fikra iliyosababishwa na mkwamba alikuwa ameingiwa na kichaa,” alisema mama huyo wakati wa mahojiano naatatizo yaliyokuwa katika ndoa yake. Ni vibaya mkewe kusema alikuwa punguani…” Mamake John aliifungukia Taifa Leo.

 

Mataifa 10 yanayoongoza kwa uhalifu wa mitandaoni, Kenya ni miongoni mwao

Kenya imemwulikwa sana kutokana na kuripoti  visa vingi vya udukuzi wa mitambo ya tarakilishi pamoja na wizi wa pesa kwenye mashine za ATM mwaka huu, idadi ya visa hivyo ikiwa takribani vitano jambo linalosemekana kuendelezwa na  wahalifu wa mitandao.

Wezi stadi wamefanikiwa kutoroka na mamilioni ya fedha kwa kudukua mashine za ATM. Udukuzi huu unajumuisha kueneza programu kwenye mitambo ya pesa na kusababisha kutoa kiasi kikubwa cha hela kwa mkupuo moja.

ATANISHO: Mume Wangu Atafute Mke Kutoka Coast Watusiane!

Akizungumza katika kongamano la uslama wa kimitandao na matumizi ya intaneti, Waziri wa usalama wa ndani Fred Matiang’i alisema kwamba kumekuwa na ongezeko la visa vya uhalifu mitandaoni, visa vya ulaghai kutoka watu bandia mtandaoni, usambasaji wa programu hasidi kwenye intaneti, udukuzi, na wizi wa kimitandaoni.

Visa hivi vimeweka Kenya katika ngazi ya juu kutokana na utovu wa usalama wa mitandaoni.

Kampuni  inayotoa huduma za kudhibiti programu hasidi Kaspersky Security Network (IT Threat Evolution Quarter Two 2019) imeorodhesha taifa la Kenya kuwa miongoni mwa mataifa 10 yanayokabiliwa na athari hiyo.

Iran inaongoza kwa asilimia 28.31, ikifuatwa na Bangladesh kwa silimia 28.1 huku Kenya ikiwa nambari 10 kwa asilimia 15.38.

Hii hapa ni orodha ya nchi zilizoripotiwa kuwa na utovu wa usalama kwenye mitandao.

Makali Ya Matiang’i: Maafisa Wawili Wasimamishwa Kazi Kwa Madai Ya Ufisadi

 

Asilimia

Nchi  %
1 Iran 28.31
2 Bangladesh 28.10
3 Algeria 24.77
4 Pakistan 24.00
5 Tanzania 23.07
6 Nigeria 22.69
7 India 21.65
8 Indonesia 18.13
9 Sri Lanka 15.96
10 Kenya 15.38

Zaidi ya visa milioni 26.6 viliripotiwa kati ya Aprili na Juni mwaka huu kulingana na  Kituo cha Kitaifa cha kudhibiti visa vya mitandaoni.

Nilipata mke wangu amebeba kila kitu na kwenda Dubai – Wycliffe

Dunia hii kwa kweli ina watu na wanyama walivalia ngozi ya binadamu.

Kesi nyingi tumeziskia mitaani ya jinsi wawili hupatana, wanapendana na huku baada ya kuteseka na kujenga familia yao pamoja shetani anaingilia mmoja wao na kuvunja kila kitu.

Mara kwa mara ni mambo na mipango ya kando lakini je ni nini husababisha wanandoa, kuharibu usiano, kuuza kila kitu na kuwacha wapendwa wao upweke?

Hilo ndilo swali analojiuliza jamaa kwa jina Wycliffe aliyesimulia masaibu yaliyomkumba baada ya kuishi kwa ndoa ya miaka tisa.

Akizungumza na mtangazaji Massawe Japanni, Wycliffe alisema kuwa alipatana na mwanadada wakiwa maskini. Wawili hao waliteseka pamoja na wakaanzisha duka lao.

Basi siku moja Wycliffe aliwabeba wanao wawili na kuelekea nyumbani kwao kutafuta shamba, mahala alipokaa kwa wiki tatu.

Alisema kuwa pindi tu aliporudi alipata yule mkewe amemuosha kila kitu na kumuacha upweke kabla ya kutorokea Dubai.

Sasa hivi, Wycliffe amelazimishwa kuishi kitongi duni cha Mathare ambapo anaishi na wanawe akijaribu kupambana na maisha.

Soma usimulizi wake,

Mimi nilioshwa, aki tulitafuta mali vizuri na wakati nilimuacha Mombasa ili niende nyumbani kwa sababu tulikuwa na duka, nilipata yuko Dubai. Alinichota baada ya miaka tisa ya ndoa na sasa mimi huskia kuwa yuko Dubai.

Hata sahii imebidi niende katika kitongoji duni cha Mathare ndio najaribu kujimudu kimaisha na nimeanza upya. Nilikuwa nimeenda nyumbani na watoto wawili na yeye akabaki na watoto wawili.

Tatizo ni kuwa nina mtoto mwingine nje ya ndoa na niliporudi nyumbani kwa majuma matatu alidhania nimeenda kurudisha yule bibi mwingine.

Alikuwa ananipangia na mimi sina habari na hata sahii huniambia yuko Dubai na akinipigia simu huwa sishiki, wacha niendelee na maisha.

Bosi mkarimu awatuza wafanyakazi 200, milioni 50 kila mmoja, Krismasi

Kampuni moja ya kuuza majumba imewashangaza wafanyakazi wake wakati huu wa Krismasi kwa kuwazawidi tuzo ambayo hawakutarajia.
Wakati msimamizi wa kampuni ya Maryland alipowapa bahasha nyekundi wafanyakazi wake katika sherehe ya likizo ya Krismasi, wengi wao hawakufahamu thamani ya zawadi iliyokuwa ndani.
Wafanyakazi hao 200 walituzwa shilingi milioni 50 kila mmoja kama zawadi kwa kazi njema kutoka msimamizi wa kampuni hiyo.
Jumla ya kima cha fedha waliyopata wote ni zaidi ya bilioni moja.
“Nilipofungua bahasha yangu, sikuamini macho yangu,” Stephanie Rdigway ambaye ni naibu maneje wa utendakazi aliiambia kituo cha habari cha CNN.
“Sikuamini niliona kile nilichoona. Sina misamiati ya kuelezea jinsi ninavyohisi, ninafuraha sana, ni maajabu.”
Kulingana na mahojiano na CNN msimamizi mkuu wa kampuni ya St. John Properties, Lawrenze Maykrantz alisema kuwa walitoa shukran kwao baada ya kampuni hiyo kuaafikia maazimio yao ya mwaka huu.
“Tulitaka kufanya jambo la kuwashukuru wafanyi kazi wetu kwa kutimiza malengo ya kampuni, na tulitaka kuwapa kitu kikubwa,” Maykrantz alisema.
Aidha aliongeza kusema kuwa kila mwajiriwa alipata bonasi hiyo kulingana na miaka aliyohudumu katika kampuni hiyo.
Kiwango kidogo zaidi alichopata mwajiriwa ambaye hata hajaanza kazi ni shilingi  elfu 10,168 huku shilingi milioni 27,453,600 ukiwa mgao mkubwa zaidi.
“Ni kweli hili ni jambo la furaha sana ambalo sijawaishuhudia katika maisha yangu. Kila mmoja amefurahi sana. Walishangilia, wakalia,wakacheka na hatakukumbatiana,”
Kampuni hiyo ya St. John Properties ambao ina matawi manane, kwa mara ya kwanza iliwalipia wafanyakazi wake tiketi za ndege pamoja na ada za hoteli kwenye sherehe ya kufunga mwaka.

(+Picha) Mchumba wa mcheshi Dr Ofweneke aonyesha ujauzito wake

Mpenzi wa mcheshi maarufu Dr Ofweneke amefunguka kuwa ana ujauzito na ana hamu kubwa sana ya kupata mtoto hivi karibuni.

Dr. Ofweneke woman pregnant

Mimi ni bikra na sipo kwenye mahusiano na jinsia ya kike, Stivo Simple Boy

Image result for ofweneke and christine

Kando na kuwa mcheshi ,Ofweneke anaendesha kipindi katika runinga.

Ofweneke pia anafahamika kama Sande Bush na ni miongoni mwa mastaa wakubwa katika tasnia ya ucheshi na uanahabari hapa nchini.

Njambi wa TRHK afunguka kuhusu mahusiano na mumewe

Mpenzi wake wa sasa ni Christine Tenderness.

Sande alipatana na mchumba huyu baada ya kutemana na Niccah The Queen.

Kwa sasa miaka mitatu imeisha tangu walipoachana.

Kuna ishara kuwa huenda Ofweneke ameamua kutulia katika ndoa na mrembo Christine.

Kupitia mtandao wa Insta, Christine alichapisha picha za ujauzito.

Tazama baadhi ya picha hizo:

Dr. Ofweneke lover pregnant

Christine pregnant

Baraza la magavana lataka hazina ya kitaifa itoe mgao wa fedha za kaunti

Baraza la magavana nchini limefika mahakama ya juu likiitaka kuiamuru hazina ya kitaifa kutoa mgao wa fedha za kaunti wa mwezi wa Novemba na Disemba kwani kucheleweshwa kunakoshuhudiwa kunaathiri utendakazi wa kaunti.

Haya ni kulingana na mwenyekiti wa baraza hilo ambaye pia ni gavana wa kaunti ya Kakamega Wycliffe Oparanya aliyesema ni kinyume cha katiba kusimamisha mgao wa kaunti bila ya mchakato wa kisheria uliotiwa sahihi na bunge la kitaifa au lile la seneti.
Amesema mgao huo wa fedha wa jumla ya shilingi bilioni 316 unapaswa kutolewa kwa serikali za kaunti ifikapo tarehe 15 ya kila mwezi.

Aidha ameilaumu hazina ya kitaifa kwa kufeli kuweka mikakati ya kuhakikisha kuwa serikali za kaunti zinapokea mgao wao wa fedha kwa wakati ufaao akisema hili limeathiri sana majukumu ya seriakali hizo.

-CALISTUS LUCHETU