PATANISHO: Tulitengana na bwana yangu 2014 lakini haoneshi hamu ya kurudiana

Rachel lituma ujumbe akiomba apatanishwe na aliyekuwa mume wake bwana Kenneth, ambaye walitengana mwaka wa 2014 akidai kuwa wamekuwa wakizungumza tangia mwaka huo.

Isitoshe anataka kuwa karibu na mumewe lakini hana uhakika kama bado wako kwa uhusiano au la.

"Tunazungumza naye lakini ile ikifika kumwambia achukue hatua turudiane kama bibi na bwana huwa anakataa." Alieleza bi Rachel.

Kile kilifanya tuwachane ni baada yake kuniwacha kwa nyumba mtoto akiwa mgonjwa na hakuwahi rudi." Wawili hao walikuwa wamejaliwa mtoto mmoja lakini aliaga dunia.

Katika harakati ya kutengana walijaliwa mtoto mwingine lakini bado Kenneth hajaonesha hamu ya wao kurudiana.

Kenneth alikata simu pindi tu Gidi alipojitambulisha.

Pata uhondo kamili.

&t=129s