PATANISHO: Tulikosana na mume baada ya jamaa kuniitisha picha za uchi wangu

Bi Val, aliomba apatanishwe na bwana Mark akisema kuwa alimkosea mume wake baada ya kupatikana akiwa anazungumza na jamaa mwingine huku wakitumiana ujumbe wa mapenzi.

Akisimulia kilichotendeka, Val alisema; Alikuja akapata message mbaya kati yangu na mwanaume mwingine na nakubali ilikuwa mbaya, lakini hakukuwa na hisia zozote kati yetu kwani sijawahi kutana naye wala kumuona.

Huyo jamaa alitoa  nambari yangu ya simu kwa mtandao wa Facebook na akanitumia ujumbe nami sikumkanya, kwa hivyo ni makosa yangu.

Aliongeza: Hata hivyo jamaa aliniambia nimtumie picha za uchi wangu lakini nikakataa. Mume wangu aliniomba simu apigie rafiki yake na akatoka nayo nje ambapo alikaa kwa mda mrefu, na hapo ndipo moto uliwaka.

Sasa mume wangu alikasirika na akatoka hata sijui kwenye yupo. Tulijaribu kuleta familia zetu pamoja lakini kila familia inaegemea upande wa mtoto wao lakini hii ndoa ni yangu.

Wawili hao wamekuwa kwa ndoa ya miaka sita na bado hawajajaliwa mtoto.

Alipopigiwa simu bwana Mark alisisitiza hana ubaya na mkewe kwani binadamu hukosea na anaelewa hilo.

"Kitu kimoja nilikusamehe kwani sote tuna doa zetu na naelewa na najua vitu zitakuwa sawa kwani sina shida nawe moyoni." Alisema.

Val alikiri kuwa hakutarajia kuwa atasamehewa kwani alimkosea vibaya lakini aliapa kuwa hatorudia alichokifanya tena.

Pata uhondo kamili katika kanda ifuatayo.