logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwalimu kuanguka na kuaga dunia kwa hali isiyojulikana

Mwalimu kuanguka na kuaga dunia kwa hali isiyojulikana

image
na

Yanayojiri02 October 2020 - 00:07
Polisi mjini Mwatate kaunti ya Taita Taveta wanaendelea na uchunguzi kubaini kilichosababisha kifo cha ghafla cha mwalimu mmoja wa shule ya upili ya kitaifa ya Bura Girl's huko Mwatate.
Inasemekana Walter Odhiambo alizirai na kuaga dunia punde tu alipofikishwa katika hospitali ya Mwatate na walimu wenzake.

Akithibitisha kisa hicho afisa mkuu wa polisi mjini Mwatate Monicah Kimani alisema ripoti ya upasuaji itaeleza rasmi sababu ya mauti ya mwalimu huyo.
Swali ni je mwalimu huyo alifanya nini na ni nini kilicho mfanya afariki?

Mwili wa mwenda zake unahifadhiwa Katika chumba Cha kuhifadhi maiti Cha hospitali ya st Joseph Shelter of hope Ikanga mjini Voi huku ukisubiri kufanyiwa upasuaji.

RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved