Wapenzi hao wawili wamekuwa wakibadilishiana ama wakitumiana jumbe za kimapenzi katika mitandao ya kijamii.
Katika picha moja ambayo iko kwenye mitandao msomaji huyo wa habari amevalia rinda la rangi nyekundu.
Atwoli aliweza kuweka picha hiyo na maandishi ya kiingereza akimwambia kuwa 'I trust you in the city of peace' yaani anamwamini aliwa katika mji huo wa amani.
Huku wakiwa katika mazungumzo hayo, Mary aliweza pia kumjibu kwa kimombo na kusema "Peaceful is an understatement! The most beautiful place I have visited so far. Can't thank you enough love."
Ni wazi kuwa wawili hao wanafurahia maisha pamoja na kama vili Kilobi alivyosema katika mahojiano yake ya awali.
Bosi wa COTU ambaye ni mume wake amemuonyesha mapenzi kweli na kumpa heshima ambayo anastahili.
"Sisi ni marafiki wazuri sana mtu yeyote ambaye yuko karibu nasi anajua kwamba sisi hatuwezi tenganishwa na chochote."Amenionyesha mapenzi kweli na heshima ambayo nastahili kupewa," Alisema Kilobi.
Atwoli aliweza kuongelea uhusiano wao na Kilobi katika runinga ya KTN (KTN screen siren) baada ya ndoa yao kuja kwenye mwangaza Oktoba mwaka jana.
"Ni mwanamke mzuri, ananijali na pia amejitolea katika uhusiano wetu, hayo ndio naweza kusema," Atwoli alisema akiwa katika mahojiano ya moja kwa moja televisheni.
Katika mahojiano yaliyopita Kilobi alisema kuwa Atwoli alisema hataki kuwa mpenzi wala kuwa na uhusiano wa kiholela.
Aliongezea kuwa aliweza kuwa na uhusiano na watu wengi lakini licha ya hayo aliweza kumpa heshima na kumuonyesha mapenzi kweli.
Haijawekwa wazi kuwa Kilobi ameenda kujivinjari Egypt lakini ukweli nikuwa Atwoli aliweza kukutana na viongozi wa (trade union) humo nchini.
Katika hoteli moja ya Intercontinental katika mji wa Cairo inayoongozwa na Mohammed Saleem.