Jinsi nilivyo mpenda Ayub Ogada asimulia mke wake

Mjane wa mwanamziki maarufu mwendazake Ayub Ogada alieleza vile walivyopatana kwa mara ya kwanza na mwana mziki huyo katika kaunti ya Nairobi.

Yvonne, 29, katika kijiji cha Nyahera kaunti ya Kisumu, alisema kuwa Ogada aliweza kuja kwa maisha yake miaka 11 iliyopita akiwa na miaka 21, naye Ogada alikuwa na miaka 52.

Nyumbani kwao kulikuwa na shida ya maji hapo ndipo Ayub aliamua kuwasaidi, na huo ulikuwa upendo wa kwanza.

Mama yake aliweza kupinga bali Yvonne aliweza kumwambia kuwa yeye yuko katika upendo na Ayub, alikuwa mwenye kutimiza ahadi.

Yvonne alisema kuwa Ayub aliweza kuaga dunia akiwa katika kochi chumbani akitazama habari katika televisheni aipendayo ya Al Jazeera.

Alikuwa katika pilkapilka zake jikoni baada ya kumpa maziwa Ayub, alipoitwa na msichana wake na kumuambia akuje kumwangalia Ayub, kwa maana alikuwa anaongea na yeye ilhali hakuwa anajibu mtoto wake.

"Nilipoenda sebuleni nilimpata akiwa amekaa macho zake zikiangalia runinga, mwili wake bado ulikuwa mmoto.

"Nilikiambia nikaenda kumuita dada wa mama wa Ayub ndipo aliponiambia Ayub tayari ashaafariki, niliweza kufunga macho kwa maana alikuwa ashaafariki," Alisema Yvonne.

Yvonne, mama wa wasichana watano, ambaye alijipea nguvu, alisema kuwa Ayub alikuwa mtu mwenye kujali na mzuri ambaye angefanya chochote ilikuona familia yake inaishi maisha mazuri.

Wakati mjane huyo alipotaja jina la marehemu tabasamu ilijaa usoni mwake. Walipatana South C kaunti ya Nairobi 2008 aliposema ulikuwa upendo mbele kwanza.

"Nakumbuka tulikuwa na shida ya maji nilipoenda kutafuta usaidizi hapo ndipo niliweza kutana Ayub ambaye alijitolea kunisaidia," Aliongea Yvonne.

Baada ya siku chache baadaye, Ayub alienda nyumbani kwa mke wake ilikumuona mamake, Kisha ndipo mamake  aliweza kulalamika kwa ajili ya miaka ya Ayub.

Ilhali Ayub aliweza kujitetea na kusema kuwa ameona ua nzuri ambalo hayuko tayari kuiachilia.

"Mengine ni historia lakini mume wangu ambaye tuko na watoto watano na yeye alikuwa mwenyekujali, mzuri na pia mkali," Aliongezea Yvonne.

Yvonne alisema kuwa Ayub amekuwa mgonjwa katika miaka miwili kisha baadaye ndipo walipojua kuwa ilikuwa ni shida ya uti ambao ulianza kutibiwa.

Aliongezea kuwa wiki mbili ambazo zilipita, Ogada alikuwa mchangamfu aliweza kuongea na marafiki, na familia mpaka walidhani kuwa amepona.

"Licha ya kuwa mgonjwa, hakuna siku ata moja ilipita kama hajaimba wimbo wake aupendao wa 'Nyatiti Koth Biro aliouimba 1993. Mara nyingi angenifunza akisema ako mahali alipo kwa sababu ya hiyo, pia alikuwa anasema 'Nyatiti'alikuwa mke wake," Alizungumza Yvonne.

Alisema kuwa walikuwa wanafanya kazi katika albamu yake ya 3, lakini Mungu aliweza kumchukua kama bado hawajamaliza.

Wimbo wake unaovuma ni 'koth biro' yaani mvua itanyesha uliochezwa katika mchezo wa kukimbia wa Olympic Rio 2016 ambapo mkimbiaji KipchogeKeino alikuwa anazawadiwa zawadi yake ya kukimbia.

Pia ameweza kuhusika katika Hollywood blockster 'the constant gardener NBC's na mengine mengi.