logo

NOW ON AIR

Listen in Live

PATANISHO: Mke wangu hunidanganya kuwa mpango wa kando ni cousin yake

PATANISHO: Mke wangu hunidanganya kuwa mpango wa kando ni cousin yake

image
na

Habari02 October 2020 - 11:27
Baba Daisy, 31, aliomba apatanishwe na mkewe bi Eunice, 28, ambaye walikosana na akambebea kila kitu kwa nyumba na kuondoka. Anadai kuwa kila anapompigia mkewe simu yeye hujibu lakini hazungumzi na sasa hajui la kufanya.

Nimekaa na my wife for four years na kuna mtu alikuwa anampigia simu na kumtumia ujumbe usiku, na nikaanza kumuuliza huyo ni nani. Kila wakati alikuwa anajibu kuwa ni cousin yake na siku moja tulikosana hadi akaangusha simu yangu sakafuni.

"Siku moja nilitoka kazini na nikapata ameondoka tayari bila kunieleza sababu yoyote." Alisema.

Wawili hao wana watoto wawili na wakekuwa kwa ndoa ya miaka minne.

Aliongeza kuwa yeye huskia wakizungumza na kila wakati huwa akimjulia hali usiku sana.

"Ule staki mambo yake staki mambo yake amenichosha sana!" Alisema bi Eunice kabla ya kusitisha mawasiliano kati yetu.

Kulingana na Baba Daisy, wawili hao walioana kirasmi na tayari wazazi wa familia hizo mbili wamekutana. Isitoshe alipata habari kuwa mkewe huwa havumilii nyumbani na kuwa huondoka na kuwacha watoto pekee yao.

"Nishawahi zungumza na yule jamaa na akazima ile laini na kubadilisha laini nyingine. Kumpigia na laini nyingine ili nimuulize mbona hajawahi kuja nyumbani tujuane huwa hazungumzi." Aliongeza Baba Daisy.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved