Hata hivyo ,kuna kanuni zinazofuatwa kuhusiana na mavazi yako . Ni muhimu kufahamu unachofaa kuvalia ukienda harusini ili kuonyesa heshima kwa wanandoa na pia kutoonekana kama doa .
Huu hapa mwongozo wa mavazi unayofaa kuyaepuka unapoalikwa harusini .
Usivalie chochote cha rangi nyeupe
Kanuni ya kwanza katika harusi zote ,wanawake hawafai kuvalia vazi lenye rangi nyeupe kwani itakuwa ni kumkosea heshima Bi Harusi na itaonekana kama ushindani kati yako na Bi harusi . Ni yeye pekee anayefaa kuonekana bayana na hivyo basi rangi nyeupe ndio huwa chagul lake .
Wanaume hawafai kuvalia tuxedo
Bwana Harusi pia anafaa kuonekana wazi kwani ni siku yake pia ,hivyo basi ni vyema kwa wageni wa kiume kuvalia suti badala ya tuxedo. Itaonekana ni kana kamba ulikuja kumpa ushindani Bwana harusi
Usionekane umevalia Denim
Denims are too casual to wear at a wedding even if you are planning to wear a blazer to make it look smart casual,it's not appropriate for a wedding.
Nguo zenye chungi(uwazi)
Sio vazi linalokubalika kwa sababu litafaa tu kwa wakati wa kujiburudisha na rafiki zako wakati wa usiku .
Nguo za rangi Nyeusi kote
Rangi nyeusi aghalabu huhusishwa na Maazishi . Kwa hivyo kuvalia rangi hii ni hatua inayoweza kuleta simanzi katika sherehe inayofaa kuwa ya vicheko .
Kaptula
wanaume wanaovalia kaptula kwenda harusi hukiuka kanuni muhimu sana . Hili linaweza tu kufanyika endapo umepewa ruhusa ya kufanya hivyo na wanaharusi . vazi hili sio rasmi na halifai kwa harusi .
Nguo zenye mikato mirefu
Harusi ni hafla ya kuonyesha miondoko na hadhi .Jaribu kuhakikisha kwamba vazi lako linawiana na mandhari ya sherehe .
Hakikisha mtindo wako unabeba na kutisha ka njia nzuri .