logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Eric Omondi alinipa shavu kimuziki, Bahati hakuweza- Madini Classic

Eric Omondi alinipa shavu kimuziki, Bahati hakuweza- Madini Classic

image
na

Habari02 October 2020 - 01:57
Madini Classic - Assumpta
Staa wa muziki nchini Madini Classic amefunguka katika kikao cha Papa Na Mastaa kuwa mchekeshaji Eric Omondi alikuwa wa kwanza kumshika mkono na kumpa moyo wa kufanya muziki. Muimbaji huyu alimtaja Eric kama nguzo muhimu katika maisha yake ya sanaa. Madini Classic aliirithi jina lake kutoka kwa babu yake ambaye alikuwa mchimbaji migodi katika kitongojiduni cha Migori.

Soma hapa:

Madini alimueleza Papa mwanzo mwisho jinsi alivyotoka kijijini na kuja Nairobi kujituma kwenye haso zake za kimziki.

"Kipindi natoka nyumbani kweli sikuwa na muziki. Nimekuja kuimba nikiwa hapa Nairobi . Muziki ulionitambulisha kwenye mainstream media unaitwa Nikaribishe. Kikawaida safari ya muziki huwa ndefu sana. Sio kitu unaweza ukabumburuka na ghafla utusue." alisema Madini.

Madini aliweza kueleza ukaribu wake na Eric Omondi na jinsi alivyomhimiza afanye muziki mkubwa.

"Eric Omondi ni mtu na ambaye anapendana sana kipaji changu. Alimuuliza Bahati huyu Madini ni nani. Bahati akamwambia kuwa mimi ni rafiki yake. So akamwambia mbona usisaidie huyu jamaa atoke kimuziki kwa sababu bahati alikuwa ashatoka na akawa mkubwa lakini inaonekana mikakati za Bahati na shughuli zikawa nyingi mpaka akasahau." Madini alimueleza Papa.

Pata uhondo hapa:

Madini alisema kuwa anatamani sana angefanya muziki na mastaa kama Sauti Sol, Alikiba na Diamond Platnumz. Kupitia kuwashirikisha kwenye ngoma, staa huyu alisema anaweza jifunza mengi kimuziki.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved