logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Niliteswa na shangazi na kubakwa na mjomba - Janet Atieno

Niliteswa na shangazi na kubakwa na mjomba - Janet Atieno

image
na CONSOLATA MAKOKHA

Habari20 June 2019 - 14:45

Muhtasari


    Bi Janet Atieno ana stori moja ya kuvunja roho sana, kwani alisimulia katika kitengo cha Ilikuaje naye Massawe Japanni jinsi alivyoteswa na kubakwa akiwa mtoto mchanga mno.

    Kama staa wa nyimbo za injili, Janet Otieno, mgeni wetu Janet Atieno pia ni msanii wa nyimbo za injili.

    Bi Janet alifichua kuwa alipitia magumu akiwa mtoto mchanga mikononi mwa shangazi yake ambaye alikuwa anamtesa licha yake kumsaidia kazi za nyumbani.

    Yule mama alikuwa anampiga kichapo cha mbwa, kipigo ambacho kilimlemaza siku moja na kufanya maisha yake kuwa magumu zaidi.

    Nilikuwa na challenges nikiwa mtoto na nikachukuliwa na shangazi yangu tukaishi naye, na alikuwa ananitesa sana usiku na mchana.

    Alinichukua nikamsaidie kazi za nyumba ingawa nilikuwa mdogo wa miaka minane na alikuwa ananipiga vibaya sana, wakati mwingine nachomeka kwa moto na hakuna jinsi ningepotea. Alisema Janet Atieno.

    Aliongeza,

    Wazazi wangu hawakujua nilichokuwa napitia kwani ni mtu walikuwa wanaamini sana na niliteswa kwa mda wa miezi mitatu.

    Baada ya mateso hayo, siku moja aliamua kukimbia mateso hayo na hapo ndipo shangazi yake alipomfungia kwa nyumba na kumpa kichapo cha mbwa kabla ya shangaziye mmoja kumchukua na kumrudisha nyumbani.

    Siku moja nilipotea na wamama fulani kwa shamba waliniona na wakakimbia kumwambia shangazi yangu na akanibembeleza nirudi. Mle nyumbani alifunga mlango na akachomoa kuni na kunipiga kichapo cha unyama.

    Nguo niliyokuwa nayo ilichomeka kwa mwili na akachukua chuma na kunigonga goti vibaya sana na hakuna aliyeniokoa.

    Baada ya kumaliza shule jirani yake mmoja alipendekeza Janet aelekee naye nyumbani kwake ili amsaidie kazi za nyumbani na kule ndipo mambo yaliharibika zaidi.

    Bwanake jirani yao alikuwa askari na yule mama akienda kazini yule bwana anarudi nyumbani na siku moja yule jamaa alimuekea bunduki kwa meza kabla ya kumbaka.

    Alijaribu kutoroka na kujificha bafuni lakini jamaa aliuvunja mlango na akambaka tena na kurudi kazini.

    Janet anasema ile ilikuwa tabia ya yule jamaa na hangemwambia yeyote kwani alikuwa ametishiwa maisha na jambo hilo liliadhiri maisha yake, na hapo akaamua kuolewa kwa mzee fulani ili apotelee shida zake.

    Niliolewa na mzee mmoja wa miaka 35, huku nikiwa 14 na baada ya miezi mitatu nikapata mimba na kujifungua mtoto wa kwanza nikiwa 16, kabla ya kujifungua wa pili miaka miwili baadaye.

    Babake Janet aliaga dunia na cha kushtua ni kuwa alipata habari baada ya miezi mitatu. Mwaka mmoja baadaye nduguye naye alifariki katika ajali ya barabarani.

    Mamake pia aliaga dunia miezi kadhaa baadaye kabla ya dadake kuondoka siku moja kwenda sokoni na hadi wa leo hakuna anayejua aliko.

    Ndugu yangu ambaye alikuwa anashikilia hati miliki za shamba alivamiwa na kukatakatwa na vijana ambao walikuwa wameongozwa na mjomba wangu.

    Isitoshe, nilipoelekea kumzika nyumbani walinizuia kumzika katika lile shamba hadi korti ilipoingilia kati na kunipa walinzi.


    RADIO JAMBO FREQUENCIES

    Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


    logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved