logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Picha chafu za Willy Paul na Nandy zilimfikia mamake? Pozze afunguka

Picha chafu za Willy Paul na Nandy zilimfikia mamake? Pozze afunguka

image
na

Habari02 October 2020 - 11:08
Fundi wa muziki na anayetamba kwa kasi Willy Paul hatimaye amefunguka mwanzo mwisho kuhusu picha chafu zilizozagaa katika mitandao ya kijamii. Picha zake na msanii wa Bongo Nandy zililipua mtandao baada ya fiesta ya Choma Na Ngoma na kuwa gumzo kubwa kitaani.

Soma hapa:

Willy Paul amesema kuwa mamake hajawahi kukutana na picha hizo kwani yeye yupo nyumbani na hanaga zile za kumfuata katika mitandao ya kijamii. Picha hizi zilikuwa za kufedhehesha ukizingatia kuwa Pozze ni staa wa nyimbo za injili. Wakenya katika mitandao ya kijamii walimchamba kweli kwa kuonekana kuasi na kumkufuru Mungu.

"Mamangu hafuatilii Show Biz zangu. Yeye yupo nyumbani. Anachokifahamu mimi ni kijana mzuri." Staa huyu alisema.

Pata uhondo hapa:

 Katika mahojiano na vyanzo mbalimbali nchini, Willy Paul alikana tetesi kuwa anatoka kimapenzi na nyota huyu wa Tanzania.

"Nandy ni dadangu mkubwa. Namheshimu sana." alijitetea Pozze.

Mwanasiasa Musalia Mudavadi alikuwa kati ya watu waliotoa maoni yao kumhusu muimbaji huyu na kumuomba ajirudi. Mwanamuziki Alaine pia alitoa kauli yake na kusema kuwa wakenya wasimkosoe kwa ukali ila wafanye hivo kwa mapenzi.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved