Eric Omondi amteka nyara Tanasha Donna

Mvunja mbavu mkenya Eric Omondi amemteka nyara mpenziwe Diamond Platinumz, Tanasha Donna.

Eric Omondi kwenye kanda ya video aliyoweka kwenye mtandao wake wa instagram unamwonyesha akimfokea Diamond Platinumz na Sultan Idris. Tanasha na Diamond wanatarajia kufunga pingu za maisha mnamo tarehe 7 Julai mwaka huu.

"Diamond, iwapo unataka kumuona mpenzio tena basi wapigie Taifa Stars, mpigie Kocha, mpigie Mbwana Samatta kisha uwaeleze wasifike  karibu na lango la Harambee stars."

Mvunja mbavu huyo ameichukua fursa hio kuwatakia Wakenya kila la heri katika mchuano wao huku akiwaogofya Watanzania. Kwa upande mwingine, watanzania wakiongozwa na mwanahabari Khatimu Naheka wameikejeli Harambee stars na kujipiga kifua kabla ya mechi hio ya kukata na shoka.

Hii leo Harambee stars inacheza na Taifa stars ya Tanzania katika mtanange ambao atakaye poteza basi yeye atakuwa ashayaaga mashindano hivo basi Harambee stars lazima washinde ili kuendelea kuwa ndani.

Takwimu ni kuwa Kenya haijawahi poteza mchezo wowote dhidi ya Watanzania nje ya Tanzania.

Video yake Eric Omondi

https://www.instagram.com/p/BzNaIQrAO7W/

Mechi baina ya Kenya na Tanzania inachezwa saa tano usiku kamili.