Sikumdhuru mpenzi wangu licha ya kumfumania na mpango wa kando - Derrick Mbugua

IMG_7541
IMG_7541
Derrick Mbugua ndiye aliyekuwa mgeni wetu siku ya Jumatatu katika kitengo cha Ilikuaje naye Massawe Japanni.

Mbugua aligonga vichwa vya habari hapo nyuma alipo rekodi mazungumzo yake na mpenziwe ambaye alimfumania akila uroda na jamaa fulani.

Wawili wao walikuwa kwa uhusiano wa miaka mitatu unusu na wamejaliwa mtoto mmoja.

Jamaa huyo anasimulia kuwa asubuhi moja alienda mpaka alipokuwa anaisha mpenziwe na alipobisha lango kuu hamna aliyemfungulia, huku ikiwa mida ya saa tisa asubuhi.

Ilimbidi akae pale nje hadi saa kumi na mbili akimsubiri mpenziwe na alipomuona alijijazia kuwa alikuwa kwa mpango wa kando. Anasema kuwa alipomkabili mpenziwe alikubali makosa yake na kusimulia kilichotokea.

Mda huu wote, Mbugua alikiwa anarekodi mazungumzo yao yote na mpenziwe hakuwa na habari.

Wakati nilimuona anaingia na ile kutembea nilijua mahali ametoka na nilipomuuliza alisema nimetoka mahali fulani kwa mtu anaitwa Chris anayeuza nguo Gikomba, ni mtu walipatana jioni akampa nambari yake. Alisimulia Mbugua.

Aliendelea,

Kupigia Chris alikuwa na wingi wa upole na akakiri kuwa hakujua alichokuwa anafanya. Kumuuliza mpenzi wangu anachotaka hakuwa na maneno ya kusema kwani alikuwa ameshtuka sana.

Mbugua anasema kuwa aliamua amsamehe mpenziwe badala ya kufanya jambo ambalo angejutia maishani.

Sababu kubwa ilifanya nimsamehe niliangalia tulipotoka, Facebook wasee wanasema nipate Chris nimmalize, marafiki wanasema tuungane tukamvamie. Lakini nikasema haifai.

Nilijaribu kumpiga nikasema hapana na nikaamua ku rekodi nikachapisha mtandaoni ili nione kama kuna mwenye amepitia hayo.