Urafiki wa kufaana . Ndio taswira inayoweza kueleza uhusiano kati ya mwanahabari Jacque Maribe na Mkurugenzi wa mawasiliano ya kidijitali katika Ikulu ,Dennis Itumbi . Maribe siku ya jumatano ‘alirudisha mkono’ kwa kumtembelea Itumbi katika makao makuu ta DCI wakati alipokamatwa kuhusiana na barua yenye madai ya kuwepo njama ya kumuua naibu wa rais William Ruto.
Itumbi amekuwa akihudhuria vikao vya kesi ya mauaji inayomkumba Maribe na mpenziwe wake wa zamani Joseph Irungu ,na masaibu yaliomfika ,jumatano yalitoa fursa kwa mwanahabari huyo kwenda kumwona .
Maribe na Jowie wanakabiliwa na kesi ya mauaji ya mfanyibiashara Monica Kimani katika nyumba za Lamuria Gardens mwaka wa 2018 . Maribe na Itumbi wana historia ndefu lakini iliyoghubika usiri kuhusu hali ya uhusiano wao sasa kwani kwa wakati mmoja walidaiwa kuwa wapenzi .