Mkusanyiko wa Habari na Matukio Muhimu ...
Oparesheni za kampuni za michezo ya kubashiri sportpesa zinaendelea ikiwemo matumizi ya nambari zake za malipo kufuatia agizo la mahakama linawaruhusu kuendelea na shughuli zao .wakili Joan Kiarie amesema agizo la serikali kuondoa nambari hizo na kuongeza ushuru ni hatua inayoavuruga biashara za michezo ya kubashiri ilhali wametekeleza sheria zote .
Mwanamke mmoja raia wa Rwanda amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela kwa kumwua mumewe ambaye ni mkenya . anashtumiwa kwa kumwua mumewe wakati walipokuwa wakingomabana baada ya marehemu kusemakwamba alitaka kuoa mke wa pili korti ilipunguza shtaka lake kuwa la mauaji ya kutokusudia .
Wazazi ndio wanaofaa kulaumiwa kwa ongezeko la visa vya wasichana wadogo kutungwa mimba huko kilifi na sio wahudumu wa boda boda . waziri wa jinsia wa kaunti Maureen Mwangovya amesema wahudumu wa boda boda wamekuwa wakitwika lawama ambayo sio yao .
Mbinu ya sasa ya mtu kutangaza wazi mali yake sio ya kuaminika na haiwezi kutegemewa katika vita dhidi ya ufisadi .afisa mkuu mtendaji wa tume ya EACC Twalib Mbarak amesema wanapendekeza marekebisho ya sheria ili kufanya zoezi hilo kuwa la kielektroniki ndiposa waweze kupata maelezo ya mapato,mali na madeni ya maafisa wa serikali .
Tume ya kupambana na ufisadi EACC imerejesha mali yenye thamani ya shilingi bilioni 2.7 katika kipindi cha miezi minne iliyopita .afisa makuu mtendaji Twalib Mbarak amesema fedha hizo zilirejeshwa kupitia njia mbadala ya kusuluhisha mizozo .
Aliyekuwa mkuu wa utumishi wa umma Francis Muthaura ameunga mkono pendekezo la kuwateua wabunge kama mawaziri . muthaura amesema kuwazuia wabunge kuhudumu kama mawaziri ni jambo ambalo limezua uhasama kati ya viongozi wa kisiasa na viongozi wengine utawala wa serikali .
Kampuni za maji taka zimehimizwa kuhakikisha kwamba maeeo ya kutupa taka hayawi karibu na vyanzo vya maji ili kuepuka kuyachafua maji . mtaalam wa afya ya umma Josephine Ofdanga amekushauri kuhakikisha kwamba unaweka dawa au kuyachemsha maji unayotumia .
Kufaulu au kufeli kwa ndoa yako hakutegemi iwapo una cheti cha ndoa .mtaalam wa masuala ya uhusiano wanjiku waititu amesema jinsi unavyojitayarisha kwa ndoa ndio msingi wa iwapo itafulu au la .
Eneo la kuosha na kurembesha magari la Pimp my ride limebomolewa baada ya mahakama kuipa city hall ruhusa ya kufanya hivyo . aeneo hilo la kusafisha magari ambalo limejengwa upya mwezi uliopita ,lilibomolewa mwendo wa saa tano usiku . maafisa wa city hall mwezi mei walikuwa tena wamelibomoa eneo hilo wakisema limejengwa bila idhini .