4 waangamia katika ajali ya barabarani

Wafanyibiashara wanne waliuawa siku ya Jumatano baada ya lori lililokuwa likiendeshwa kwa kasi kuwakanyaga katika barabara kuu ya Nairobi – Nakuru karibu na eneo Soko Mjinga.

Watu wengine 10 walijeruhiwa, watano kati yao malipata majeraha mabaya na kupelekwa katika hospitali ya Kaunti ndogo ya Naivasha.  Shughuli za kawaida katika soko hilo zililemazwa huku polisi wakifika kuchukua miili ya walioaga na kuvuta mabaki ya magari yaliohusika katika ajali hiyo.

Kulingana na mfanyibiashara katika soko hilo, Jackson Mwangi, kwanza lori hilo liligonga matatu iliokuwa ikibeba abiria na gari lingine dogo.

“Tukio lilifanyika haraka sana,” alisema

OCPD wa Njabini Charls Rotich alisema kwamba dereva wa lori hilo alitoweka na polisi wameanzisha msako kumtafuta.