Patanisho: Alitoka nyumbani bila sababu mwaka 2017

Bi. Emily alipiga simu akitaka kupatanishwa na mumewe,Fredrick aliyemwacha mwaka wa 2017. Wawili hawa wana mtoto mmoja mwenye umri wa miaka mitatu na nusu.

 "Tulikuwa tumeishi vizuri na mume wangu lakini mwaka wa 2017 nilianza kuona tabia za kiajabu kutoka kwakee. Alianza kuja nyumbani kama amechelewa sana kitu saa nane usiku na akifika anasema ameshiba. Siku moja nilimwambia  kimchezo kama amechoka na mimi achukue virago vyake na aende zake. La kustaajabisha alichukua vitu na akaenda na hadi wa leo hajawahi kurudi."

Emily amekua akizungumza na mumewe hata ikafikia kuwa mumewe anamtumia pesa kila wakati akimwitisha licha ya kwamba mumewe huyo amekataa kurudi nyumbani.

Tulipompigia bwana Fredrick simu alikataa kuzungumza nasi kwani alisema kuwa atampigia mkewe simu baadaye.