Wakenya wamkashifu Betty Kyallo kwa picha aliopiga na watoto wa mitaani

Betty Kyallo, siku ya Ijumaa aliweka mtandaoni picha akila chakula cha mchana na watoto wa kuranda randa mitaani, kwa lengo la kupiga jeki kipindi chake , Weekend with Betty.

Katika picha kwa kurasa zake mitandaoni, mtangazaji huyo wa runinga anaonekana akijiburudisha kwa chakula cha mchana na watoto hao  Kevin na Ras, katika mkahawa mmoja maarufu katikati mwa mji wa Nairobi.

"I spent a day with these amazing street kids, Kevin and Ras. It was so special. They showed me where they sleep, bathe, eat, buy sniffing glue, places we couldn't go and places we could go to, everything. It's just one of my best pieces," Alieleza kwenye photo.

Hata hivyo, huku baadhi ya wananchi wakimpongeza baadhi yao walikosoa hatua hiyo wakisema kwamba alikuwa tu anatumia hatua hiyo kunadi umaarufu wa kipindi chake.

Wengi wao walimtaka Betty kuwapa watoto hao suluhisho la kudumu kuboresha maisha yao.

Haya ni baadhi ya maoni yao:

"So did you do anything about it or you just enjoyed listening to their stories?" Davis Haven posted.

"You should donate to shelters, clothing and food. It's not good to post them on social media," Karani Martin opined.

"Apart from spending time with them and buying them food, what difference did you make in their lives? Did you give them a better place to stay? Or it's just selfie things!" Kevin Odhis queried.

"Hope your kindness to them was not only for tonight's show...find them a bedsitter and I hope they get kind donors," Rajab Muli suggested.